TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) inatarajia kuweka kambi maalum ya upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo mkoani Dar es salaam na mikoa ya jirani katika kuadhimisha siku ya wanawake Duniani Machi 8, 2024.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano ,Anna Nkinda imesema wataalamu wa JKCI, Hospitali ya Dar Group  iliyopo Tazara  Wilaya ya Temeke  watatoa huduma za tiba mkoba zijulikanazo kwa jina la Dk Samia Suluhu Outreach services  kwa kufanya kambi hiyo maalum.

“Upimaji  huu unafanyika kwa watoto na watu wazima kuanzia tarehe 2 hadi 3,2024 kuanzia saa mbili kamili asubuhi  hadi saa 10 kamili jioni katika hospitali ya JKCI Dar  Group.

Aidha amesema katika kambi hiyo kutakuwa na wataalamu wa lishe ambao watatoa elimu  ya lishe bora ambayo itawapa wananchi uelewa na kufuata mtindo  bora wa maisha  na kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo ambayo yanayweza  kuepukika kwa kuafuata ushauri wa kitaalamu.

“Tunawaomba wananchi mjitokeze kwa wingi kupima afya zenu  kujua kama mnamatatizo ya moyo ili kuanza matibabu mapema  kwa atakayegundulika kuwa mgonjwa kwa taarifa zaidi wasiliana  kwa simu namba 0787941606 Dk Samweli Rweyemamu  na 0674179036 Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI) Hospitali ya Dar Group.

a lishe ambao watatoa elimu  ya lishe bora ambayo itawapa wananchi uelewa na kufuata mtindo  bora wa maisha  na kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo ambayo yanayweza  kuepukika kwa kuafuata ushauri wa kitaalamu.