JPM ainoa safu yake

DAR ES SALAAM

NA MWANDISHI MAALUMU

 

Julai 28, mwaka huu, Rais John Magufuli, alifanya uteuzi na uhamisho wa viongozi wa mikoa, wizara na wilaya.

Amefanya mabadiliko hayo baada ya baadhi ya viongozi kustaafu, kuteuliwa kushika nafasi nyingine na wengine kuachwa.

 

 Wakuu wa Mikoa

 

 1. Ally Salum Hapi (aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni) ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa. Anachukua nafasi ya Amina Masenza ambaye amestaafu.

 

 1. Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera. Anachukua nafasi ya Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu ambaye amestaafu.

 

 1. Albert Chalamila ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya. Anachukua nafasi ya Amos Gabriel Makala ambaye amehamishwa na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi.

 

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga amestaafu.

 

 1. Brigedia Jenerali Nicodemas Elias Mwangela ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe. Anachukua nafasi ya Luteni Mstaafu Chiku Gallawa ambaye amestaafu.

 

Wakuu wa mikoa ambao hawakutajwa katika mabadiliko haya wanaendelea na nyadhifa zao kama kawaida.

 

Makatibu Tawala wa Mikoa

 1. Kessy Maduka ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma. Anachukua nafasi ya Rehema Madenge

 

 1. Aboubakar Mussa Kunenge ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam. Anachukua nafasi ya Theresia Mmbando.

 

 1. David Kafulila ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe.

 

 1. Denis Bandisa ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita. Anachukua nafasi ya Selestine Gesimba

 

 1. Happiness Seneda William ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa. Anachukua nafasi ya Wamoja Dickolagwa.

 

 1. Abdallah Mohamed Malela ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi.

 

 1. Rashid Kassim Mchata ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma. Anachukua nafasi ya Charles Pallangyo.

 

 1. Missaile Mussa ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara.

 

 1. Caroline Albert Mthapula ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara.

 

 1. Dk. Jilly Elibariki Maleko ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara. Anachukua nafasi ya Alfred Luanda.

 

 1. Christopher Derek Kadio ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza. Anachukua nafasi ya Kamishna wa Polisi Mstaafu Clodwing Mtweve.

 

 1. Eric Shitindi ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe. Anachukua nafasi ya Jackson Saitabau.

 

 1. Profesa Riziki Salas Shemdoe ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma. Anachukua nafasi ya Hassan Bendeyeko.

 

 

Makatibu Tawala waliohamishwa

 

 1. Rehema Madenge aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, amehamishiwa katika Mkoa wa Lindi.

 

 1. Theresia Mmbando aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam amehamishiwa katika Mkoa wa Pwani.

 

 

Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu

 

 1. Profesa Joseph Buchweshaija anakuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji. Anachukua nafasi ya Prof. Elisante ole Gabriel.

 

 1. Andrew Wilson Massawe anakuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.

 

 1. Profesa Elisante ole Gabriel anakuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo).

 

 1. Dk. Jim James Yonazi anakuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano)

 

 1. Edwin Paul Mhede anakuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

 

Wakuu wa Wilaya

 

 1. Jerry Cornel Muro anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.

 

 1. Frank James Mwaisumbe ni Mkuu wa Wilaya ya Longido. Anachukua nafasi ya Daniel Geofrey Chongolo.

 

 1. Patrobas Katambi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma.

 

 1. Mwanahamisi Athuman Mukunda anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Bahi. Anachukua nafasi ya Elizabeth Simon Kitundu.

 

 1. Daniel Geofrey Chongolo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.

 

 1. Sara Msafiri Ally aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang amehamishiwa Wilaya ya Kigamboni. Anachukua nafasi ya Hashim Shaibu Mgandilwa.

 

 1. Said Mkumba anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukombe. Anachukua nafasi ya Josephat Paulo Maganga

 

 1. Josephat Paulo Maganga amehamishwa na kuwa Mkuu wa Wilaya ya Geita. Anachukua nafasi ya Herman Clement Kapufi.

 

 1. Kanali Patrick Norbert Songea amekuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato. Anachukua nafasi ya Shaaban Athuman Ntarambe.

 

 1. Rashid Mohamed Mwaimu ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa. Anachukua nafasi ya Kanali Shaban Ilangu Lissu

 

 1. Kanali Simon M. Anange anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kasulu.

 

 1. Luteni Kanali Michael Masalama Ngayalina anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe. Anachukua nafasi ya Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti.

 

 1. Lengai ole Sabaya anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai.

 

 1. Hashim Shaibu Mgandilwa ahamishiwa Wilaya ya Ruangwa. Anachukua nafasi ya Joseph Joseph Mkirikiti.

 

 1. Elizabeth Simon Kitundu anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Babati. Anachukua nafasi ya Raymond Hieronimi Mushi

 

 1. Joseph Joseph Mkirikiti anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang. Anachukua nafasi ya Sara Msafiri Ally.

 

 1. Mary-Priska Winfred Mahundi anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Chunya. Anachukua nafasi ya Rehema Manase Madusa.

 

 1. Ngollo Malenya ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ulanga. Anachukua nafasi ya Jacob Joseph Kassoma.

 

 1. Moses Joseph Machali amekuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu.

 

 1. Dk. Severin Mathias Lalika amekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela.

 

 1. Dk. Philis Meshack Nyimbo amekuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana. Anachukua nafasi ya Mary Onesmo Tesha.

 

 1. Dk. Philemon Sengati ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magu. Anachukua nafasi ya Hadija Rashid Nyombo.

 

 1. Kanali Lucas Boniphace Magembe anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe. Anachukua nafasi ya Estomih Francis Chang’ah.

 

 1. Zainab Rashid Mfaume Kawawa anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo. Anachukua nafasi ya Majid Hemed Mwanga.

 

 1. Jokate Mwegelo amekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe. Anachukua nafasi ya Happiness Seneda William.

 

 1. Sophia Kizigo anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo. Anachukua nafasi ya Luckiness Adrian Amlima.

 

 1. Jasinta Venant Mboneko amekuwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga. Anachukua nafasi ya Josephine Rabby Matiro.

 

 1. Rahabu Mwagisa Solomon ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni.

 

 1. Pasacas Muragiri amekuwa Mkuu wa Wilaya ya Singida. Anachukua nafasi ya Elias Choro John Tarimo.

 

 1. Komanya Eric Kitwala ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora.

 

 1. Kisa Kasongwa amepelekwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe.

 

32:  Gift Isaya Msuya ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora.

 

 

 

Taarifa ya Ikulu ilisema tarehe ya kuapishwa kwa Wakuu wa Mikoa, Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa itafanyika tarehe 1/082018  siku ya jumatano.

Wakuu wa Wilaya wataapishwa na Wakuu wao wa Mikoa kwa utaratibu utakaopangwa.