Na Suzy Butondo,JamhuriMedia,Shinyanga

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini ambaye pia ni naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Patrobas Katambi amewaomba viongozi wa CCM na Serikali kushirikiane naye kufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo na kutatua kero mbalimbali za wananchi ili wapate maendeleo katika jimbo hilo.

Hayo ameyasema leo Machi 13, 2024 wakati akizungumza na wananchi wa Jimbo la Shinyanga katika Kata ya Kitangili, ambapo amesema ili kuweza kuijenga Shinyanga ni vizuri kuwa wamoja na kushirikiana katika kufanyakazi za uchocheaji maendeleo, kuwahudumia wananchi na kuwaondolea manung”uniko .

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi akizungumza na wananchi wa Kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga.

Katambi amesema wananchi wanatarajia kuona maendeleo makubwa katika maeneo yao, ambayo mengi tayari yamefanyiwa kazi, barabara zilikuwa hazipitiki madaraja yalikuwa hayapo, lakini kwa sasa barabara zinapitika, zahanati, mashule bado kero ndogo ndogo ambazo zinatakiwa kutatuliwa, ambapo ameahidi kuzifanyia kazi wakati wowote.

“Niwaombe wananchi muwaamini viongozi wenu kuanzia ngazi za mitaa, kata madiwani mbunge na Rais kwa kuwaletea miundombinu ya barabara zahanati, mashule na ninaamini tutaendelea kuboresha huduma mbalimbali za kijamii,”amesema Katambi.

“”Leo naomba niwatajie michango mbalimbali nilioitoa katika jimbo langu kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2024,kwa taasisi za dini na jamii, ikiwemo kwenye Chama cha Mapinduzi na jumuiya zake kwa ajili ya makongamano mabaraza na ugeni mbalimbali wa jumuiya zetu jumla milioni 41.7” amesema Katambi.

Aidha amesema Januari hadi Desemba 2023 aliwawezesha wajasiliamali 910 kupata semina na kuwawezesha gharama za nauli na chakula jumla shilingi milioni 75, ikiwa ni pamoja na kuwezesha wajasiliamali na viongozi kupata semina ya matumizi ya majiko ya gesi na kugawa majiko ya gesi 1,680 pamoja na nauli jumla ya Shilingi milioni 92.4.

Viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi wakimsikiliza mbunge wa Jimbo la Shinyanga.

“Jimbo langu linakata 17, ambapo kata zote tayari nimegawa fedha kutoka mfuko wa jimbo kwa ajili ya kuchochea utekelezaji wa miradi ya maendeleo 2024, kuboresha huduma zote za kijamii zikiwemo huduma mbalimbali za kijamii katika kata zote jumla Shilingi milioni 62.6.

“Machungu yangu ni kuhakikisha kila mmoja tunaungana pamoja na kuhakikisha masikini anatendewa haki, tajili anatendewa haki, usaliti na roho mbaya sio mzuri tuungane kwa pamoja ili tuweze kuijenga Shinyanga yetu., mimi kazi yangu ni kufanya maendeleo, hivyo niwaombe viongozi wenzangu tuwatumikie wananchi wetu na tuhakikishe katika uchaguzi tunapata ushindi kwa kishindo”ameongeza Katambi.

Katambi alimuomba Mwenyekiti wa CCM Shinyanga asimame imara na kamati yake siasa ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma zinazohitajika kwenye jamii na kwuwataka madiwani kusimamia miradi mbalimbali ya serikali inayoendelea kutekelezwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu.

Wananchi wa Kata ya Kitangili mlManispaa ya Shinyanga wakimsikiliza mbunge wa jimbo hilo

Kwa upande wake diwani wa Kata ya Kitangili Mariam Nyangaka amesema yuko pamoja na mbunge katika kuhakikisha maendeleo yanapatikana katika kata ya Kitangili kwani mpaka sasa kuna mabadiliko makubwa katika barabara na madaraja kulikuwa na shida kubwa lakini kwa sasa wananchi wana amani.

Baadhi ya wananchi wa Kitangili akiwemo Vedastina Nyakonga ameipongeza serikali pamoja na viongozi wa CCM kwa kusimamia vizuri na kuleta maendeleo ya barabara kwani ikinyesha mvua ilikuwa shida watoto kwenda shule kutokana na barabara kujaa maji lakini kwa sasa barabara zinapitika bila wasiwasi.

Diwani wa Kata ya Kitangili Mariam Nyangaka akizungumza kwenye mkutano wa mbunge uliofanyika katika kata hiyo

By Jamhuri