Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, amewataka Waislamu kuzingatia mafundisho ya Mtume Muhammad (SAW) hususan kuhusu uchamungu na tabia njema.

Kinana ameyasema hayo jana wakati wa hafla ya mashindano ya Kuraani tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Faraja Foundation ya jijini Dar es Salaam.

“”Tunaagizwa na Kuraani, pia tunaagizwa na Mtume wetu (Muhammad – S A.W) kuwa kila Mwislamu anapaswa kuzingatia mambo mawili lakwanza ‘takwa’ (uchamungu) na lapili ‘akhlaki’ tabia njema).

“Kwahiyo ukizingatia ‘takwa’ ukazingatia na maadili mema hakuna namna utapotoka, itakuwa hakuna haja hata ya sisi kuwa na wasiwasi kwamba maadili mabaya yanaweza yakatupitia,” alisema Kinana.

Aidha, aliwahamasisha Waislamu nchini kuwapeleka watoto wao madrasa wakajifunze imani na maadili ya dini yao na kumjua Mwenyezi Mungu.

By Jamhuri