Serikali ya Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya watu watatu na makampuni tisa kwa kusaidia usafirishaji wa mafuta ya Iran kuelekea China.
Kampuni nne zina makao yake Hong Kong na nne nyengine ziko katika Falme za Kiarabu kwa huku kampuni ya tisa ikiwa na makao yake Oman.
Haya yanafanyika siku chache kabla Rais Donald Trump kufanyaziara mjini Beijing ambapo atakutana na kiongozi wa China Xi Jinping.
Kwengineko spika wa bunge la Iran Mohammad Bagher Ghalibaf amesema jeshi la nchi hiyo liko tayari kutoa kile alichokiita “funzo” kwa yeyote atakayeanza uchokozi.


