Mwenyekiti wa chama cha upinzani Chadema, Freeman Mbowe katika mahakama ya Kisutu

Viongozi sita wa CHADEMA wanatarajiwa kuachiliwa kutoka kizimbani baada ya kulipa dhamana, siku ya Alhamisi.

Viongozi hao wa chama cha CHADEMA, akiwemo mwenyekiti Freeman Mbowe, walishtakiwa kwa uchochezi ,kuleta vurugu na kuandamana mwezi wa Februari mwaka huu.

Alhamisi iliopita, mahakama ya hakimu mkazi Kisutu iliwapatia dhamana viongozi hao sita lakini kusema kuwa watasalia rumande hadi leo tarehe 3 Aprili ambapo wataletwa mahakamani kukamilisha masharti ya dhamana.

Wanasiasa hao hawakuletwa mahakamani katika uamuzi wa dhamana yao huku afisa wa magereza akiiambia mahakama ni kutokana na gari lililotakiwa kuwasafirisha kuja mahakamani hapo kuwa bovu.

Miongoni mwa mashtaka waliyosomewa ni pamoja na maandamano yaliyosababisha kifo cha mwanafunzi wa chuo cha NIT Akwilina Akwiline.

Wanashtakiwa pia kuendelea kufanya mkusanyiko usio halali wilayani Kinondoni shtaka linalowakabili washtakiwa wote.

Wakati huo huo, Jeshi la polisi Tanzania, inaendelea kumshikilia mjumbe mwingine wa chama hicho Halima Mdee.

 

By Jamhuri