Na Mwandishi Wetu,Jamhurimedia

Asia Kibishe (27),mkazi wa Kijiji cha Nyarututu,wilayani wilayani Chato Mkoa wa Geita amejinyonga kwa kipande cha kanga kwa madai mumewe Fabian Shija (23) Mkazi wa Nyarututu,kumtuhumu kuiba sh,10,000.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi, Septemba 15, 2022 Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Henry Mwaibambe amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Kamanda Mwaibambe amesema kuwa marehemu alijinyonga hadi kufa kwa kipande cha kanga kutokana na mumewe kumtuhumu kuiba Sh 10,000 zilizokuwa chumbani kwao.

Kamanda amesema mwili wa mwanamke huyo umekutwa ukining’inia kwenye mti ulio karibu na nyumbani kwao na chanzo cha tukio hilo ni mgogoro kati yake na mumewe .

Amesema mwanamke huyo baada ya kutuhumiwa kuiba Sh.10,000 kitendo hicho kilimkasirisha na kuamua kujinyonga.

By Jamhuri