Na Dvid John,Tabora

Mkulima wa zao la Tumbaku wilayani Sikonge Mkoani Tabora Masoud Kilyamanda amempongeza Rais wa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa harakati anazozifanya za kuhakikisha kuwa sekta ya kilimo inanufaisha walengwa hususani zao la tumbaku ambalo makampuni ya ununuzi wa zao hilo yanazidi kuongezeka na kilimo hicho kuonekana chenye tija.

Amesema kuwa anamshukuru Rais Dkt Samia Suluju Hassan kwa kuruhusu makampuni ya nje kuja nchini kununua zao la tumbaku jambo ambalo limewafanya wakulima waanze kuwa na maisha bora na kuendelea kuwa na imani zaidi na Serikali ya Awamu ya Sita.

Pia amesema kama serikali itaendelea kutoa ruzuku kwenye mbolea wakulima watafanya mabadiliko makubwa sana ya kimaendeleo hasa Mkoa wa Tabora ambako zao la tumbaku linalimwa kwa wingi ukizingatia zao hilo ni zao la kibiashara na lakimkakati.

Kilyamanda ameyasema haya wilayani sikonge mkoani Tabora jana baada ya kutembelewa na waandishi wa Habari kwenye mashamba yake yaliyopo kwenye vijiji vya Lufwisi kata ya Igigwa ,pamoja na Kijiji cha Igarula ,kitongoji cha Mmembi.

” Ndugu waandishi wa habari kama mnavyoona wenyewe hapa ni zaidi ya hekari 300 na nimeweza kuajiri vijana zaidi ya 20 na wanalipwa mshahara hapa karibu sh.milioni 25 hivyo ni uwekezaji mkubwa na ndio maana nasema nashukuru Taasisi za fedha kama Azania Benki wameweza kuniamini na kunipa mkopo wa Trector.” amesema.

Nakuongeza kuwa “naziomba Taasisi zingine kuwa karibu na wakulima hasa mkulima mkubwa kama mimi waje kunitembelea wajionee wenyewe uwekezaji huu .kwani naamini wanapoona Kwa macho ni rahisi kumkopesha mkulima.

Amesema licha ya kufanya vizuri kwenye kilimo cha tumbaku lakini anatamani pia kufanya shughuli za ufugaji wa samaki hivyo anaiomba serikali kupitia Wizara ya kilimo chini ya Waziri Hussein Bashe kunisaidia ili aweze kupata malambo ya kuhifadhi maji.

Pia kilyamanda ameongeza kuwa ukiachia mbali kilimo ,na ufugaji lakini pia anajishughulisha na ufugaji ambapo hadi kufikia Sasa anang’omba 80 na huko kote ameweza kutoa ajira Kwa vijana ambao wanafanya kazi huko nakwamba ndoto yake nikuwa mkulima mkubwa zaidi na mtu ambaye ataendelea kuisaidia Serikali kutatua tatizo la ajira.

Naye mkulima mwingine wa zao la tumbaku Mkoani humo Shija Madowo akizungumzia baadhi ya changamoto zinazowakabili wakulima Amesema changamoto ni kuwa ni kipindi wanapofikia kwenye ukaushaji wa tumbaku kwani ili tumbaku ikauke inahitaji kunii au miti ya kuni jambo ambalo wakati mwingine linaleta shida .

Amesema kuwa wakati wakukausha tumbaku wamekuwa wakilazimika kulipia senikalini ambapo kwa hekta moja wanalipa dola 200 za kimarekani na kuongeza kuwa badala ya kupungua gharama inazidi kuongezeka mpaka kufikia 50,000 nakuwaomba waandishi wa Habari kusaidia kupaza sauti ili serikali iweze kuwasaidia

Madowo amefafanua kuwa kilimo cha tumbaku gharama yake ni kubwa mno hasa kwa upande wa mbolea ambapo mfuko mmoja wa mbolea ni dola 70 sawa sawa na shilingi 170,000 za kitanzania jambo ambalo kwa mkulima wa kawaida hawezi kumudu gharama hizo

.“Naiomba serikali ijaribu kuangalia kwenye changamoto za mbolea hususani tupate ruzuku ya pembejeo ya tumbaku NPK ,kwa kweli tunashukuru kwa upande wa mwaka jana tulipata ruzuku ya mbolea ya kutosha ndiyo maana kwa msimu huu tumevuna mazao ya kutosha,”amesema Mkulima huyo.

Amesema kuwa anaelekeza ombi lake kwenye wizara ya kilimo kutatua changamoto ya mbolea ya ruzuku ya zao la tumbaku aina ya NPK, na kutumia nafasi hiyo kumwomba Waziri Hussein Bashe awasaidie wakulima hao wa zao la tumbaku ili waendelee kulima zao hilo kwa wingi waweze kunufaika.

Aidha Kwa upande wa familia ya Masoud wameishukuru serikali kwa kuendelea kuwa pamoja na wakulima jambo ambalo limefanikisha kunyanyua kipato cha wananchi kupitia kilimo huku wakidai kuwa mwanzo familia hiyo ilikuwa masikini lakini leo wametajirika kupitia kilimo.

Pamoja na mambo mengine familia hiyo imeshauri vijana wengi waige mfano wa mkulima huyo kwa kulima kwa bidii kwani sekta ya kilimo ndiyo mhimili wa uti wa mgogngo kwa mtanzania ambapo familia nyingi zinanyanyuka kupitia sekta ya kilimo.

By Jamhuri