IMEELEZWA kuwa zaidi ya siku 130 katika Mto Ruaha Mkuu hujatiririsha maji kutokana na uharibifu uliofanywa ndani ya Bonde la Ihefu.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Kituo cha Wanahabari Watetezi wa rasilimali na Taarifa (MERISA),Habibu Mchange wakati wa Kupitia Kongamano la Wahariri na Wadau wa Uhifadhi, Mazingira na Utunzaji wa Vyanzo vya Maji lililpfanyika mkoani Iringa leo Desemba 19, 2022.

Mchange amesema kuwa uharibifu huo unatajwa kufanywa na baadhi ya wananchi kwa sababu ya maslahi binafsi na kusababisha kero kwa wakulima na wafugaji.

‘Shughuli za kibinadamu zinazofanywa na wananchi wachache katika Bonde la Ihefu ndio chanzo cha kukauka kwa Mto Ruaha.

“Uharibifu huo umesababisha wanyama wengi katika hifadhi ya Taifa Ruaha kufa na wengine kuambukizwa magonjwa mbalimbali kutokana na kukosa maji ya kutosha,” amesema Mchange.

Mchange ameongeza kuwa zaidi ya asilimia 60 ardhi ya Tanzania imeharibika na asilimia 16 ya nchi ya Tanzania ni jangwa kutoka na uharibifu wa kimazingira unaofanywa na baadhi ya wananchi.

“Mto Ruaha na mito mingine kama hatua za haraka hazitachukulia basi tutavuna mabua kutokana na uharibifu unaoendelea” amesema Mchange