Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia,Mbeya

Watu nane wamefariki dunia baada ya kontena la mchanga kufeli breki na kuligonga basi la Super Rojas lilikikuwa likitokea Mbeya kwenda Njombe.

Kamanda wa Polisi mkoani humo Urlich Matei amethibitisha kutokea tukio hilo leo iliyotokea katika eneo la Shamwengi karibu na kituo cha mafuta Inyala mkoani hapo.

Amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni baada ya kontena la mchanga kufeli breki lilikwenda na kuligonga basi la Super Rojas lililokuwa likitoka Mbeya kwenda Njombe.

Amesema baada ya kugonga basi hilo, liliendelea kushuka zaidi na kuligonga gari lingine aina ya benzi na kusababisha vifo na majeruhi kadhaa ambao idadi yao haijajulikana haraka.

“Waliopoteza maisha ni watu nane japokuwa bado idadi rasmi haijajulikana ila baadaye taarifa ya daktari itaeleza kwa ujumla, ila majeruhi wamesambazwa kwenye hospitali tofauti ikiwamo Igawilo na Mkoa,” amesema Matei.

By Jamhuri