Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ametoa ufafanuzi wa mambo 10 muhimu kwa mstakabali wa maendeleo na ustawi wa jamii katika Mkoa huo na Taifa kwa Ujumla.

RC Chalamila akiongea na Waandishi wa Habari Ofisini kwake ametoa ufafanuzi na mikakati ya Serikali ya Mkoa kama ifuatavyo:

Halihalisi ya uendelezaji wa masoko katika mkoa RC Chalamila amesema kumekuwa na changomoto kubwa katika Masoko mengi ambapo yako makundi ya watu wachache wasiowaadilifu ambao wanaendesha masoko na Serikali haipati chochote, uamuzi wa Serikali ni kurudisha masoko hayo kusimamiwa na Halmashauri ndio maana hivi karibuni nimevunja uongozi wa Soko la Mabibo hata hivyo tayari timu ya wataalam imeundwa kupita katika masoko yote ya Mkoa na kuleta taarifa ya hali halisi ya masoko hayo.

Migogoro ya Ardhi Mkoa wa Dar es Salaam umekuwa na migogoro mingi ya Ardhi ambayo husababishwa na vikundi vya watu, makampuni ya uuzaji na kupima Ardhi pia kufoji nyaraka mbalimbali tena wengine wanashirikiana na viongozi wa Umma hili halikubaliki Serikali iko timamu katika kuchukua hatua Stahiki kwa wote wanaochangia migogoro hiyo.

Usalama wa watu na mali zao Hali ya usalama katika Mkoa iko shwari licha ya kuwa hivi karibuni kulitokea na vijana wachache vingunguti walishazibitiwa na vyombo Mkoa uko salama, “lazima tulinde amani ya Mkoa kwa kuwa ndio kitovu cha biashara, Diplomasia na ni Mkoa wenye watu wengi tusikubali amani itoweke” amesemaChalamila

Mabasi yaendayo kasi Rais Mhe Dkt Samia ameendelea kuboresha miundombinu ya usafiri hususani Mwendokasi ameshatoa pesa za kupanua barabara kutoka Ubungo kuungana na njia nane kimara mwisho pia miundombinu imeendelea kuboresha katika maeneo mbalimbali ya Mkoa na sasa Utekelezaji wa awamu ya tatu unaendelea.

Usambazaji wa maji kumekuwa na mpango kabambe wa kuboresha miundombinu ya maji ili kuondoa Changamoto ya maji DSM tayari Serikali inajenga bwawa kubwa la kidunda na uchimbaji wa visima vya maji unaendelea Kigamboni na hivi karibuni ataanza ziara ya kukagua miradi ya maji katika mkoa huo.

Wafanyabishara wadogo machinga kurudi katika maeneo yasiyo rasmi mfano eneo la Mbagala wamekua wakifanya biashara katika miundombinu ya mwendokasi hivyo amewataka viongozi wa machinga kuwahamasisha kufanya biashara kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na si vinginevyo

Wafanyabishara kulipa Kodi za Serikali kila mfanyabiashara anayetakiwa kulipa Kodi anapaswa kulipa Kodi Serikali imekuwa ikitekeleza miradi mingi ya maendeleo hivyo namna pekee ya kukamilisha miradi hiyo ni kulipa kodi ili Serikali ipate mapato.

Hali ya migomo migomo isiyo na tija RC Chalamila amesema migomo migomo sio njia sahihi ya kufikia Suluhu za matatizo yetu ” ebu jiulize endapo Daktari, Mwalimu au kundi lolote likigoma nini kitatokea? nitoe rai njia ya mazungimzo ni njia sahihi kufikia Suluhu ya matatizo yetu” Alisema Chalamila

Barabara eneo la Viwanda Kigamboni Serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya barabara maeneo mbalimbali ya kimkakati barabara hiyo kuelekea kisarawe II iko katika hatua ya tenda ili ijengwe kwa kiwango cha Lami.

Usafi RC Chalamila amewataka wakazi wa Mkoa na watu wengine wanaingia na kutoka kila kukicha katika Mkoa huo kuhakikisha Mkoa unakua safi, wafanyabishara, Taasisi na watu wengine kuacha kutupa taka ovyo na amezitaka Halmashauri kutenga bajeti za kuwa na Dampo na kuwalipa wakandarasi wa taka kwa wakati.

Aidha Albert Chalamila amesema ataendelea kutoa taarifa kwa umma mara mara za utekelezaji wa miradi na mipango ya Serikali kwa masilahi mapana na ustawi wa jamii pia kuanzia mwezi ujao atafanya mikutano mikubwa katika kila Wilaya kueleza Dira na mwelekeo wa viongozi wa Mkoa, kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

By Jamhuri