Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia,Dodoma

HADI kufikia Juni 30, mwaka huu Ofisi ya Msajili wa Hazina imekusanya mapato yasiyo ya kodi ambayo yanajumuisha gawio, michango ya asilimia 15 ya mapato ghafi na mapato mengineyo kiasi cha Sh. Bilioni 852.98 sawa na asilimia 109.5 ya lengo.

Hayo yameelezwa jana jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Umma Ofisi ya Msajili wa Hazina, Lightness Mauki,wakati akitoa taarifa kuhusu Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za taasisi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

Mauki amesema kuwa ufanisi huu umechangiwa na kuimarisha usimamizi, ufuatiliaji na tathmini ya uwekezaji wa mitaji ya Umma, hatua za makusudi zilizochukuliwa na Serikali katika kukuza mapato na kudhibiti matumizi .

Mauki amesema katika kutekeleza majukumu yake ya kisheria pamoja na mambo mengine Msajili wa Hazina ana jukumu la kukusanya mapato yasiyo ya kodi ambayo yanajumuisha gawio, michango ya asilimia 15 ya mapato ghafi na mapato mengineyo.

Mauki, Ofisi imeendelea kutekeleza jukumu hilo kwa ufanisi ambapo mapato yamekuwa yakiimarika mwaka hadi mwaka.

“Kufikia tarehe 30 Juni 2022, OMH ilikuwa imekusanya kiasi cha Sh.bilioni 852.98 sawa na asilimia 109.5 ya lengo lengo lilikuwa kukusanya Sh. bilioni 779.03 na asilimia 33.5 zaidi ya kiasi kilichokusanywa 30 Juni 2021 ambacho kilikuwa ni Sh. bilioni 638.87.Huu ni ufanisi mkubwa, unaotia moyo na ambao haujawahi kufikiwa”amesema Mauki.

Amesema kuwa wanamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan na wataendelea kuendelea kutekeleza majukumu yetu ya msingi kwa umahiri ili ufanisi huu uwe endelevu.

Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Umma Ofisi ya Msajili wa Hazina, Lightness Mauki,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa kuhusu Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za taasisi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 leo Oktoba 26,2022 jijini Dodoma.

Ofisi ya Msajili wa Hazina ina wajibu wa kusimamia na kuhodhi uwekezaji wa mali zote za umma ikijumuisha Uwekezaji wa hisa katika Taasisi na Mashirika ya Umma na katika kampuni ambazo Serikali inamiliki hisa au ina maslahi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

Aidha, Mauki ameongeza Ofisi ya Msajili wa Hazina ina jukumu la kusimamia shughuli zote za Taasisi, Wakala na Mashirika ya Umma nchini. Majukumu ya MWH yameainishwa katika kifungu cha 10 cha Sheria ya Msajili wa Hazina.

Kuhusu upanuzi wa kiwanda cha sukari cha Kilombero amesema kuwa serikali ni mbia katika Kiwanda hicho ambapo ina umiliki wa asilimia 25 kupitia Msajili wa Hazina.

“Kutokana na kuendelea kukua kwa mahitaji ya sukari nchini sambamba na ongezeko la malighafi kutoka kwa outgrowers (wakulima wadogo wanaolima kandokando ya Mto Kilombero) kumekuwa na uhitaji wa kupanua kiwanda cha sukari Kilombero ili kutimiza mahitaji haya.

“Uwekezaji huo unatarajiwa kuzalisha sukari tani 144,000 ambazo zitaongeza uwezo wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero kuzalisha sukari hadi kufikia tani 271,000 kutoka tani127,000 za sasa”amesem

By Jamhuri