Tusipotoshe kauli tukaiharibu nchi
Siku ya Ijumaa ya Agosti 9, mwaka huu nilipigiwa simu na marafiki zangu wawili kwa nyakati tofauti na kutoka maeneo tofauti. Simu ya kwanza ilitoka maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam na simu ya pili ilitoka jijini Mwanza kule Usukumani. Katika simu zote mbili hizi ujumbe ulikuwa mmoja “…Brigedia Jenerali, umesoma gazeti [nalihifadhi] la Jumatano…