Mauaji yakimbiza ajuza, vikongwe

Baadhi ya watu, wakiwamo ajuza na vikongwe katika vijiji vya Kongolo na Shilingwa, Wilaya ya Magu mkoani Mwanza wamekimbia makazi yao wakihofu kuuawa. Miongoni mwa waliokimbia ni Sophia Pondi (54) aliyevamiwa nyumbani kisha wavamizi hao kumpigilia msumari tumboni. Wakazi wa Kijiji cha Shilingwa; Tabiza Genge (72), Kazungu Luhwegula (82) na Lukanya Kidai wamehamia kwa Diwani…

Read More

IGP Sirro: Kuna urasimu mkubwa umiliki wa silaha

Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali (IGP) Simon Sirro, ametoa mwito kwa wananchi wenye kustahili kuwa na silaha kuomba wamilikishwe ili wajilinde dhidi ya wahalifu. IGP Sirro alitoa kauli hiyo alipozungumza na waandishi wa habari, ambapo pamoja na mambo mengine alizungumzia tukio lenye ukakasi la kutekwa mfanyabiashara Mohammed Dewji (Mo), Oktoba 11, mwaka huu….

Read More

Viongozi wa dini fichueni waovu – RC Mghwira

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, amewataka viongozi wa dini kuwafichua walioua viwanda vilivyokuwa mhimili wa uchumi wa mkoa huo pamoja na viongozi waliohusika kufilisi mali za vyama vya msingi na ushirika. Mghwira ameyasema hayo wakati akizindua kamati ya maridhiano ya  mkoa ambayo inaundwa na viongozi kutoka madhehebu mbalimbali ya dini pamoja na watendaji wa…

Read More

Mwandishi auawa ubalozini

Mwanahabari, Jamal Khashoggi, aliuawa katika vita katika Ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul, runinga ya taifa hilo imesema ikinukuu uchunguzi wa awali. Naibu Ofisa Mkuu wa Idara ya Ujasusi, Ahmad al-Assiri na Mshauri Mkuu wa Mwanamfalme Mohammed Bin Salma Saud al-Qahtani walifutwa kazi kufuatia kisa hicho. Wakati huohuo, Uturuki imeapa kufichua maelezo yote kuhusu mauaji…

Read More

Wanaume washirikishwe uzazi wa mpango

Tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma, utoaji wa mimba zisizopangwa na uzazi usiofuata kanuni za uzazi wa mpango umepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na matumizi ya njia za uzazi wa mpango. Matumizi hayo ya njia za uzazi wa mpango yameleta tija katika familia nyingi, japo mimi kama daktari nakiri kuwa bado elimu zaidi inahitajika ili…

Read More