Humphrey Hesron Polepole Balozi na Mkuu wa Kituo cha Uwakilishi – Havana Nchini Cuba amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Miguel Díaz-Canel Bermúdez Rais wa Jamhuri ya Cuba.

Baada ya kuwasilisha hati Balozi Polepole amekuwa na mazungumzo mafupi ambapo amempa salamu za mshikamano kutoka kwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, naye Rais Díaz-Canel amemhakikishia ushirikiano mkubwa na ambao umejengwa katika misingi imara na waasisi wa mataifa yetu Mwalimu Julius Nyerere Rais wa kwanza wa Tanzania na Kamanda Fidel Castro Kiongozi wa Mapinduzi ya Cuba.

Wakati uo huo Balozi Polepole amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Wizara ya Elimu ya Cuba ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya siku ya kimataifa ya Kiswahili itakayoadhimishwa Julai 7, 2023. Uongozi wa Wizara ya Elimu ya Cuba umeridhia kuwa sehemu ya Maandalizi ya maadhimisho hayo.

Imetolewa na,Ubalozi wa Tanzania – Havana