Vurugu zimeendelea huko ukanda wa gaza na ukingo wa magharibi ambapo zaidi ya wapalestina thelathini wamejeruhiwa katika makabiliano na polisi wa Israel

Hii ni kufuatia Rais Donald Trump kutangaza kuutambua mji wa Yerusalemu kuwa mji mkuu wa Israel.

Wakati huo huo Marekani imeionya Palestina dhidi ya maamuzi yake kutotaka kukutana na makamu wa rais marekani ,Mike Pence katika kikao ambacho kilipangwa kufanyika mapema mwezi huu.

Waandamanaji wamechoma matairi na kurusha mawe huku maafisa usalama wa Israel wakifyatulia wandamaanaji hao hewa ya kutoa machozi na risasi za mpira.

Huko Gaza kundi la kiislamu la Hamas limeitisha intifada au mapambano. Omary Shakir mkuu wa shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch katika eneo la Isreal na Palestina yupo mjini Ramala.

Kwa upande wake Naibu waziri anayehusika na masuala ya Diplomasia wa Israel Michael Oren amesema tangazo la Rais Trump imeifanya Israel iwe na furaha na ameongeza kuwa mamlaka ya Israel ilitarajia vurugu kutoka kwa wapalestina.

Vurugu zaidi zinatarajia kuendelea huku kikao cha dharara baraza la usalama la umoja wa mataifa kinatarajiwa kutoa maamuzi mazito kuhusu tamko hilo la rais Donald Trump.

 

By Jamhuri