JE, Mahakama ya Juu zaidi itaweka historia nyingine inapojitayarisha kusikiliza na kuamua ombi la urais la Kiongozi wa Azimio Raila Odinga?

Hilo ndilo swali kuu ambalo wengi wanatafakari huku Mahakama Kuu nchini ikijiandaa kusikiliza hoja kutoka kwa kundi la mawakili kuhusu ombi la kupinga ushindi uliokabidhiwa Naibu Rais William Ruto baada ya Wakenya kupiga kura tarehe 9, Agosti 2022.

Odinga alipinga matokeo ya urais na ana hadi leo saa nane kuwasilisha ombi lake. Mkenya mwingine yeyote ambaye hakuridhika na matokeo ya uchaguzi anaweza pia kuwasilisha ombi hilo.

Odinga, mgombea mwenza wake Martha Karua, na kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka jana walisalia na msimamo, wakisisitiza kwamba azma yao katika mahakama ya upeo itaonyesha ulimwengu jinsi ushindi wao ‘uliibiwa’

By Jamhuri