Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) Dkt. Sifundo Moyo wakati wakivuta kamba kuashiria ufunguzi wa Jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika (PAPU Tower) lililopo eneo la Philips Jijini Arusha tarehe 02 Septemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) Dkt. Sifundo Moyo, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye pamoja na viongozi wengine wakati akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika (PAPU Tower) lililopo eneo la Philips Jijini Arusha tarehe 02 Septemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye, Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) Dkt. Sifundo Moyo pamoja na viongozi wengine wakati wakitazama na kusikiliza maelezo juu ya Jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika (PAPU Tower) lililopo eneo la Philips Jijini Arusha tarehe 02 Septemba, 2023.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha Wageni katika Ofisi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) Dkt. Sifundo Moyo mara baada ya kufungua Jengo la PAPU Tower, Philips Jijini Arusha tarehe 02 Septemba, 2023.

By Jamhuri