Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mkoa
wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian mara baada ya kuwasili katika Chuo cha VETA cha Wilaya ya Igunga mkoani Tabora tarehe 17 Oktoba, 2023.

VYUO 64 vya Ufundi Stadi (VETA) vitajengwa nchi nzima, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mipango ya serikali kujenga vyuo hivyo kila wilaya nchini.

Hayo yamesemwa leo Oktoba 17, 2023 na Rais Samia Suluhu Hassan katika hafla ya kuweka jiwe la msingi katika chuo cha VETA wilayani Igunga, ikiwa ni ziara yake ya kikazi Mkoa wa Tabora.

“Chuo hiki ni sehemu ya jitihada ya serikali kuwapa vijana elimu ya amali, ili waweze kujiajiri au kuajiriwa,” amesema Rais Samia.

Muonekano wa Majengo ya Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora tarehe 17 Oktoba, 2023.

Rais Samia amesema mikakati ya serikali ni kuhakikisha kila mkoa nchini kunakuwa na chuo cha VETA cha Mkoa, lengo ni kuwawezesha wananchi kuwa na ujuzi wa kutumia fursa zilizopo katika maeneo yao.

Rais amewataka wananchi wa Tabora kulima kwa juhudi, kwani masoko ya mazao yao ni ya uhakika na kwamba serikali inaendelea na juhudi za kuwatafutia masoko nje ya nchi, na pindi masoko yanapokuwa changamoto serikali itayanunua mazao yao.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia vikundi vya
ngoma za asili mara baada ya kuwasili katika Chuo cha VETA cha Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora tarehe 17 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akicheza pamoja na Kwaya ya Watoto wa Shule ya Msingi Majengo mara baada ya kuwasili katika Chuo cha VETA cha Wilaya ya Igunga mkoani Tabora tarehe 17 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mkoa
wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian mara baada ya kuwasili katika Chuo cha VETA cha Wilaya ya Igunga mkoani Tabora tarehe 17 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mara
baada ya kuweka jiwe la Msingi Ujenzi wa Chuo cha VETA cha Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora tarehe 17 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mara baada ya kuweka jiwe la Msingi Ujenzi wa Chuo cha VETAcha Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora tarehe 17 Oktoba, 2023. tarehe 17 Oktoba, 2023.

By Jamhuri