Na Dotto Kwilasa,JamhuriMedia, Dodoma

Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa CPA.Amos Makalla
amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM)kikiwa kinatarajia kuadhimisha miaka 48 tangu kuanzishwa kwake kinatarajia kuwatambulisha Rasmi wagombea wake kwa wanachama katika nafasi ya ngazi ya Urais na Makamo kwa wanachama wake Januari 5,2025 jijini Dodoma.

Makalla amezungumza hayo leo January 3,2025 Jijini hapa wakati amezungumza na waandishi wa habari ambapo ameeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi .

“Tunatarajia kuwa na jambo kubwa,tutawatambulisha wagombea wa Urais na Makamu wa Rais Tanzania bara na Tanzania Visiwani,CCM inafanya sherehe yake ya kutimiza miaka 48 tangu kuzaliwa kwake na katika tukio hilo jambo kubwa ni kuwatangaza wagombea ambao walipitishwa na mkutano mkuu kugombea nafasi ya Urais na makamu ya Rais kwa Tanzania bara pamoja na mgombea Urais kwa Tanzania visiwani, “amesema

Mbali na hayo Makala amefafanua,” Ijulikane kuwa kwa sasa CCM inawatangaza wagombea wao kwa wana CCM na muda ukifika watambulishwa kwa wananchi ili kufanikisha suala la kutimiza masuala ya uchaguzi kikatiba lakini sasa hivi ni muda wa wanachama wa CCM kutambilishwa wagombea wao,”amesema.

Kutokana na hayo amewataka wana CCM wote kutoka Mikoa jirani na walioko katika Dodoma kuhakikisha wanafika katika uwanja wa Jamhuri kwa ajili ya kushuhudia sherehe hizo .

“Niwakaribishe watanzania wote walioko Dodoma na nje ya Dodoma wana CCM na wasiokuwa wana CCM kufika katika uwanja wa Jamhuri kwa kuwa milango itakuwa wazi kuanzia saa 12 alfajiri hii siyo ya kupewa kadi kila mtu anakuja,”amesema.