Ratiba ya 16 Bora Kombe la Dunia 2018

Alhamisi ya June 28 tumeshuhudia michuano ya Kombe la Dunia 2018 hatua ya makundi ikimalizika kwa Afrika kupoteza timu zote 5 katika hatua ya makundi kutokana na kukosa point za kutosha kuingia hatua ya 16 bora.

Katika hatua hiyo ya makundi timu zote 5 za Afrika zimeyaaga mashindanl hayo kutokana na kukosa alama za kuwavusha kwenye hatua hiyo ya makundi.

Timu 16 zilizofuzu hatua ya 16 bora ni Ubelgiji, England, Argentina, Colombia, Japan, Croatia, Hispania na Ureno.

Nyingine ni Brazil, Switzerland, Mexico, Ufaransa, Uruguay, Urusi, Denmark na Sweden, hatua hiyo ya 16 bora itaanza kesho Jumamosi ya June 30 na kufikia tamati Jumanne ya July 03.

Hii hapa ratiba kamili ya 16 bora

Jumamosi ya June 30-2018
Uruguay vs Portugal saa 17:00 jioni

France vs Argentina saa 21:00 usiku

Jumapili ya July 01-2018
Span vs Russia saa 17:00 jioni

Croatia vs Denmark saa 21:00 usiku

Jumatatu ya July 02-2018
Brazil vs Mexico saa 17:00 jioni

Belgium vs Japan saa 21:00 usiku

Jumanne ya July 03-2018
Sweden vs Switzerland saa 17:00 jioni

Colombia vs England saa 21:00