Na Mwandishi Wetu,JahuriMedia

Serikali imeeleza kuwa, mchakato wa marekebisho ya sheria zinazosimamia sekta yahabari haujakwama.

Kauli hiyo imetolewa na Gerson Msigwa, Msemaji wa Serikali alipozungungumza na mwandishi wa habari hii kuhusu maendeleo ya mchakato huo, tangu kufanyika kikao cha kwanza cha wadau wa habari na serikali tarehe 11-12 Agosti 2022.

Mwandishi alitaka kujua maendeleo ya mchakato huo baada ya serikali na wadau kufanya kikao cha pamoja tarehe 11-12 Agosti 2022 ambapo baadhi ya vipengele walikubaliana na vingine viliwekwa kiporo.

“Subirini mtapewa taarifa” Msigwa alimueleza mwandishi huku akisitiza “…lakini (mchakato) unakwenda vizuri.”

Wadau wa habari chini ya Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa (CoRI) alikuwa na matumaini ya mapendekezo hayo kufikishwa katika Bunge la Septemba na kusoma kwa mara ya kwanza.

Mpaka sasa, serikali imeeleza kupeleka muswada wa sheria ya kulinda taarifa binafsi katika Bunge linaloendelea sasa (Bunge la Septemba), hata hivyo bado ipo kimya kuhusu mapendekezo ya wadau ya mabadiliko ya sheria ya habari

By Jamhuri