Rais wa Marekani amesema kuwa mazungumzo yanaendelea “kwa utaratibu na kwa njia yenye kujenga,” na kusisitiza kuwa hana haraka ya kufikia makubaliano ya kuvimaliza vita baina yake na Iran.
Trump amesema siku ya Jumapili kupitia mtandao wa Truth Social kwamba licha ya mazungumzo hayo kuendelea lakini hana haraka ya kufikia makubaliano na kuwaagiza wapatanishi wa Marekani kutokimbilia kufikia makubaliano kwa kuwa bado wana muda.
Amesema hayo huku maafisa wa Iran wakieleza kwamba bado kuna vizingiti vikubwa vinavyopaswa kutafutiwa majibu, na hususan suala la mali za Iran zinazozuiliwa kwenye mataifa mengine, ambazo Tahran inataka ziachiliwe.

