……………………………………………………………………………….

Simba SC wameizamisha Yanga SC katika mchezo wa Ligi Kuu baada ya kuichapa mabao 2-0 Ligi Kuu ya NBC uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Simba SC walianza kwa kasi ya ajabu na mnamo dakika ya 2 Beki Kisiki Henock Inonga aliwanyanyua mashabiki wake akifunga bao safi kwa kichwa akimalizia Krosi ya Shomari Kapombe.

Baada ya kupata bao hilo Simba waliendelea kuishambulia Yanga na dakika ya 32 Kiungo mshambuliaji aliyekubarika kwa mashabiki Kibu Denis alipigilia msumari wa pili kwa shuti kali lililomshinda Diarra.

Kwa ushindi huo Simba wamefikisha Pointi 63 na kupunguza ‘gape’ la Pointi na kubaki alama tano huku kila timu ikibakiwa na mechi nne Ligi imalizike.

Yanga wanabaki na Pointi zao 68 ili wawe mabingwa wa Ligi msimu huu wanahitaji kushinda mechi tatu ili wafikishe Pointi 76 ambazo Simba akishinda mechi zake zote atakomea pointi 75 .

By Jamhuri