WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene,akizugumza wakati  akifungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa  viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) unaofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU CP Salum Rashid Hamduni,akielezea lengo la Mkutano wa Mkuu wa mwaka wa  viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) unaofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bi. Neema Mwakalyelye akitoa neno la utangulizi wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka 2023 wa Viongozi wa TAKUKURU  unaofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma,

Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani), wakati wa  Mkutano Mkuu wa mwaka wa  viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) unaofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamisha wa Polisi, Salum Hamduni akimkabidhi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene tuzo ya kuthamini mchango wake katika mapambano dhidi ya rushwa wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka 2023 wa Viongozi wa Taasisi hiyo unaofanyika kwa siku tatu  jijini Dodoma.

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua  Mkutano Mkuu wa mwaka wa  viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) unaofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma.

…………………………………………………….

Waziri  wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene,amesema bado yapo malalamiko mengi ya wananchi kuwepo kwa vitendo vya rushwa katika ofisi za umma hali inayosababisha wengi wao kushindwa kuzifikia huduma wanazozihitaji.

Waziri Simbachawene,ameyasema hayo leo Novemba 20,2023 wakati akifungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa  viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) unaofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma.

Waziri Simbachawene amesema kuwa  rushwa ndogondogo bado  zipo na zinawakera wananchi hivyo lazima kuwa na mikakati ya kuhakikisha zinazuiliwa.

“Bado suala la rushwa ndogondogo ni tatizo sana kwa wananchi wetu na huko ndiko yapo malalamiko mengi ya watu kutokana na rushwa hiyo kuwanyima fursa ya kupata huduma.

“Huduma hizo ni pamoja na elimu ngazi za chini kati hadi vyuo vikuu, lakini pia huduma za afya,kodi na leseni ambako kumewekwa utaratibu mgumu na ukilitimba katika utoaji wa huduma ili tuu watu watoe rushwa ndipo wahudumiwe”amesema Mhe. Simbachawene

Aidha amesema kuwa kuna haja ya kutengeneza sheria za kuwashughulikia viongozi walioshiriki katika masuala ya rushwa  wanapostaafu ili kutoa funzo kwa viongozi wengine.

”Mtu anapostaafu kama alishiriki katika uozo lazima ashughulikiwe tukifanya hivyo tutakuwa tunatoa somo kwa viongozi wengine.Tusipo shughulikiana tutakuwa hatusemi ukweli kwa Taifa letu  kwasababu rushwa bado ni tatizo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP Salum Rashid Hamduni, amesema kuwa katika mwaka wa fedha uliopita taasisi hiyo imefanikiwa kuokoa sh. bilioni 171.9

“Mafanikio tuliyoyapata katika mwaka wa fedha uliopita TAKUKURU kwa kutumia vyombo vya uchunguzi imefanikiwa kuokoa zaidi ya sh.bilioni 171 fedha hizo kama zisingefuatiliwa zingeishia mikononi mwa watu na kufanyiwa ubadhilifu,”amesema CP Hamduni

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule,amempongeza Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuonyesha uongozi imara kwa vitendo.

“Tunampongeza Rais Dk.Samia kwa kuendelea kuonyesha uongozi imara kwa vitendo ambapo amekuwa akiongeza bajeti ya taasisi hizi zinazosimamia haki na demokrasia ili zifanye kazi kwa weledi,”amesema

By Jamhuri