Na Dotto Kwilasa,JamhuriMedia,Dodoma

SPIKA wa Bunge ambaye Pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani(IPU) Tulia Akson ametoa rai kwa Waandishi wa Habari nchini kuielimisha Jamii kuhusiana na mabadiliko ya Tabianchi kutokana na kuwepo kwa athari mbalimbali zilizotokana na mafuriko.

Tulia ametoa rai hiyo Leo Mei2,2024 Jijini Dodoma kwenye Maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani wakati akizungumza na Waandishi wa Habari,Wadau wa Habari wakiwemo Viongozi wa Serikali na Asasi za kiraia.

Amesema Watu milioni16 nchini wanategemea rasilimali za Pwani hivyo waandishi wanategemewa kuokoa rasilimali hizo hasa kwa kutoa elimu kwani uharibifu wa mazingira haufanyikia Tanzania Bara pekee bali hata ukanda wa Pwani.

Pamoja na hilo ,amewataka Waandishi wa Habari kuhakikisha wanazingatia suala la usawa wa kijinsia katika kuripoti Habari za uchaguzi ili kutenda haki kwa Wagombea.

Kwa upande Wake Waziri wa Habari,Mawasiliano na teknolojia ya Habari Nape Nnauye .amewataka wanahabari kuhamasisha watanzania kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi huku akiwataka Waandishi wa Habari kutenda haki wakati I wa kuripoti taarifa za wagombea bila kujali vyama vyao.

Aidha Waziri Nape Amelishukuru Bunge kwa mapendekezo ya Sheria ya Habari huku akisema kuwa Changamoto kubwa I liyopo ni uchumi wa vyombo vya habari hivyo Kama Serikali wataliangalia suala hilo kwa Kulipa madeni ili viweze kuimarika.

“Yapo mambo mengi yamefanyika kuzingatia uhuru wa Vyombo vya Habari hivyo kuna mabadiliko ili kuhakikisha uhuru wa habari unaimarika,Uhuru wa Vyombo vya habari sio tu uhuru wa Demokrasia bali ni demokrasia yenyewe,”Amesema

Awali Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC)Deogratius Nsokolo,amesema kuwa Waandishi Ni Afya ya ustawi wa jamii na ni chachu katika maendeleo hivyo wana imani na serikali kuendelea kulisikiliza kundi la wanahabari nakuzifanyia kazi changamoto ambazo zimekuwa zikiwakwaza kwenye kazi ya Habari.