Na Magrethy Katengu,JamuhuriMedia,
Dar es Salaam

TAASISI ya Mama Ongea na Mwanao kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wametoa Baskeli za 250 kwa watoto wenye mahitaji maalumu (Walemavu) 250 ili kuwasaidia kutimiza ndoto zao za kupata elimu .

Akizungumza na Waandishi Wahabari Juni 11, 2024 jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa taasisi hiyo Steve Nyerere amesema baadhi ya wazazi wamekuwa wakipitia wakati mgumu mara baada ya kujifungua watoto wa aina hiyo kwani wanaume huwatelekeza Wake zao.

“Kuna Wanaume ni Wazembe katika kulea Watoto wenye Ulemavu hufikiria kuwa na mtoto mwenye Ulemavu ni mkosi dhana hiyo waachane nayo Mungu hapendezwi hata kidogo mtoto akiwa na hana ulemavu anamdai wake akiwa na ulemavu ni mwanamke mtoto “amesema l Mwenyekiti wa Taasisi Ongea na Mwanao Steve Nyerere.

Nyerere ameongeza kwa kusema kuwa mtoto mwenye uhitaji maalumu haimzuii kupata Elimu kwani hiyo ni Mipango ya Mungu nasio mkosi hivyo jamii ni budi kuondoka na dhana hiyo ya kuwanyanyapaa.

“Sisi tunahitaji kupeleka mahitaji kwa wenye uhitaji popote walipo hivyo tunaomba taasisi nyingine zituunge mkono”amesisitiza Steve Nyerere.

Katibu wa taasisi Ongea Na mwanao Evon Sherry amesema taasisi hiyo imetembelea mikoa mitano na bado mikoa miwili kwa ajili ya viti mwendo kwa wahitaji.

Hivyo kampeni ya “Baskeli ya Shule ya Mama” inalenga kumsaidia mtoto mwenye uhitaji kupata elimu na afike shule kwa wakati muafaka.

“RaisDk.Samia Suluhu Hassan anawasaidia wakina mama katika sekta ya Afya,Maji lakini Sisi tumeamua kumtua mama mtoto mgongoni” Alisema Evon Sherry.

Naye Mzazi wa Mtoto aliyepewa baiskeli Yusufu Mohamedi ameshukuru sanaa kwa msaada huo ambapo hapo awali ilimlazimu kuamka asubuhi kumbeba mtoto mgongoni na kumpeleka shule hivyo sasa hata kama atakuwa na shughuli nyingi wanafunzi wenzie wanaweza kumsaidia kumsukuma na kurudi naye nyumbani.