Mafanikio yoyote yana sababu (24)

Padre Dk Faustin Kamugisha Kuwajali wateja ni sababu ya mafanikio. Mteja ni kama damu muhimu kwa uhai wa biashara yako au shughuli yako. Kanuni ya msingi kwa yeyote anayehudumia mteja ni mteja kwanza. Mteja ni mfalme. Inaweza kukuchukua miezi kumpata mteja na sekunde moja kumpoteza. Usipowajali wateja wako, mtu mwingine atawajali. Yatafakari maneno ya Mahatma…

Read More

Mafanikio yoyote yana sababu (20)

Mafanikio yoyote yana sababu (20) Padre Dk Faustin Kamugisha Kutenda au kuchukua hatua ni siri ya mafanikio.  Ahadi ni wingu, kutenda ni mvua. Ni methali ya Kiarabu. “Kutenda ni ufunguo wa msingi wa mafanikio yote,” alisema Pablo Picasso (1881-1973), mwandishi wa maigizo, mpaka rangi na mchongaji wa sanamu wa Hispania. Matendo yana kauli kuliko maneno. Watu…

Read More

MAFANIKIO YOYOTE YANA SABABU (19a)

Padre Dk Faustin Kamugisha Uvumilivu au ustahimilivu ni siri ya mafanikio. Uvumilivu ni kuanguka mara 99 na kuinuka mara ya 100. Katika msingi huu Julie Andrews alisema, “Uvumilivu ni kushindwa mara 19 na kushinda mara ya 20.” Matone yanayodondoka mwishowe humomonyoa mwamba. Ni methali ya China. “Kama Columbus angerudi alikotoka, hakuna mtu yeyote ambaye angemlaumu….

Read More

Mafanikio yoyote yana sababu (14)

Na Padre Dk. Faustin Kamugisha   Kuwa na ndoto na kuzifanyia kazi ni siri ya mafanikio. Watu wanaofanya vitu vikubwa wanaota ndoto kubwa. Watu wanaofanya vitu vingi sana wanaota ndoto nyingi sana.   “Unaamini katika ndoto? Ukitaka ndoto zako ziwe ukweli wa mambo usipitilize katika kulala! Usiache ndoto ziwe jinamizi,” alisema Henrietta C. Mears (1890–1963)…

Read More

Mafanikio yoyote yana sababu (11)

Na Padre Dk. Faustin Kamugisha   Shukrani ni sababu ya mafanikio. “Kama unataka kugeuza maisha yako, jaribu kushukuru. Maisha yako yatabadilika kwa kiasi kikubwa sana,” alisema Gerald Good. Ingawa tuna mioyo midogo, lakini inaweza kubeba jambo kubwa nalo ni shukrani. Hesabu mafanikio usihesabu matatizo. Hesabu baraka, usihesabu balaa. “Afadhali kupoteza hesabu wakati unahesabu baraka zako kuliko kupoteza…

Read More