Na Jumanne Magazi, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Tanzania imetajwa kuongoza miongoni mwa nchi nne zisizo na usalama wa viivuko Barani Afrika, kwa mujibu wa tafiti za kidunia imefahamika.

Hayo yamebainishwa kwenye mkutano wa Kimataifa wa Wadau wa Usalama wa Vivuko barani Afrika, unaofanyika jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Dk Khalid Salum Mohammed.

Amesema lengo la mkutano huo ni kuangalia sababu zinazochangia kuwepo kwa ajali nyingi baharini na katika mazingira mengine ya usafiribwa majini,na kutatua changamoto zake.

Aidha Dkt Khalid amezitaja aina za changamoto za ajali ambazo zinaweza kutokea kwenye njia za usafiri hususani baharini kuwa ni pamoja na ajali za moto, ajali za kuzama kwa vyombo na ajali za kuvamiwa na maharamia na watekaji ikiwemo ugaidi.

Amesema mkutano huo umehudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka ndani ya Bara la Afrika na Dunia kwa ujumla ukiwa na lengo kutathimini hali ya usalama wa Pwani, ambapo miongoni mwa wataaalam wa maswala vyombo vya bahari wakishirikiana na Shirika la umoja wa matafa Uhamiaji (IMO) ambapo ndio waandaaji wa mkutano huo.

Katika hatua nyingine Waziri huyo amewataka wananchi wanaofanya shughuli zao za kiuchumi ndani ya bahari na maziwa kufuata sheria zinaoelekeza matumizi salama ya vyombo vya usafiri majini ili kupunguza ajali na madhara yanayoweza kuhepukika, kwa maisha Yao na jamii kwa ujumla.

Aidha Dk, Khalid amesema kutokana hali ya mazingira salama na bora ya Pwani ya bahari ya Hindi hususani Tanzania Jambo ambapo limepelekea nchi yetu kuwa mwenyeji wa mkutano huo.

Katika hatua nyingine Khalid amesema wajumbe wa mkutano huo wameadhimia kuchukua hatua madhubuti na za pamoja zitakazo saidia kupunguza changamoto zinazopelekea kuongezeka kwa ajali nyingi kwa vyombo vya usarishaji baharini.

Vilevile DK, Khalid amesema Serikali zote mbili zinaendelea kusisitiza wananchi wote hususani wanaotumia vyombo vya usafiri kufuata Sheria na miongozo iliyopo na kukazia kuanzia sasa kutakuwa na umakini kwa wale wote watakao kaidi kufuata Sheria za ndani na zile za Kimataifa.

Mwisho Wlwaziri huyo amezishukuru taasisi zote zilizofanikisha kufanyika kwa Mkutano huo ikiwemo TASAC na Wizara za Uchukuzi ya Tanzania Bara na ile ya SMZ.

By Jamhuri