Na. Ramadhani Kissimba na Farida Ramadhani, WF – Nairobi.

Tanzania inatarajia kushika nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji mbadala (Alternative Executive Director) katika Kundi la Magavana wa Afrika Mashariki katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kuanzia mwezi Agosti, 2024.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba ameyasema hayo kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wakati wa Mkutano wa kawaida wa Magavana wa Kundi la Nchi za Afrika Mashariki ambao ni wanachama wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ikiwa ni maandalizi ya Mikutano ya Mwaka 2024 ya Bodi ya Magavana (Mawaziri wa Fedha kutoka nchi wanachama) wa Benki hiyo inayofanyika Jijini Nairobi nchini Kenya.

Dkt. Mwamba alieleza kuwa Benki ya Maendeleo ya Afrika imeweka utaratibu wa mzunguko wa uongozi katika Nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki ambao ni Mkurugenzi Mtendaji na Mshauri na kwa upande wa Tanzania kunakuwa na Mkurugenzi Mtendaji mbadala (Alternative Executive Director).

Kamishna Msaidizi wa Fedha za Nje kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Robert Mtengule akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji anayewakilisha Kundi la Afrika Mashariki na Kati katika Bodi ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Bw. Jonathan Nzayikorera katika Mkutano wa kawaida wa Magavana kutoka Kundi la Nchi za Afrika Mashariki ambao ni wanachama wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ikiwa ni maandalizi ya Mikutano ya Mwaka 2024 ya Bodi ya Magavana (Mawaziri wa Fedha kutoka nchi wanachama) inayofanyika Jijini Nairobi nchini Kenya.

‘’Katika mkutano huu tumezungumzia pia mzunguko wa viongozi ambao ni Mkurugenzi Mtendaji na Mshauri na sisi Tanzania kuanzia mwezi Agosti, 2024 tutashika nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji Mbadala katika Benki hiyo ambaye atakuwa anachukua nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji anapokuwa anapata udhuru’’ alisema Dkt. Mwamba.

Aidha, Dkt. Mwamba alisema kuwa mkutano huo ulijadili kuhusu mabadiliko ya tabia nchi ambayo hivi karibuni yamekuwa yakisababisha maafa mbalimbali na kukubaliana kuanzishwa kwa mfuko wa maafa ambao utakuwa unasaidia nchi zitakazo athirika na mabadiliko hayo ikiwemo mvua zisizotarajiwa za El nino.

“Tumejadili pia kuhusu mabadiliko ya tabianchi na namna ya kuongeza mtaji lakini pia nchi zilizopata majanga ya mafuriko yaliyosababishwa na mvua nyingi zilizojitokeza mwaka huu pia itakuwa ajenda itakayojadiliwa katika Mkutano Mkuu”, aliongeza Dkt. Mwamba.

Mkutano wa Kundi la Nchi za Afrika Mashariki ambao umeshirikisha Wajumbe kutoka nchi tisa (9) ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Ethiopia, Somalia, South Sudan, Eritrea na Seychelles, ni utangulizi wa Mkutano wa 59 wa Mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) unaofanyika Nairobi, Kenya.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Shaabani wakiwa katika Mkutano wa Kundi la Afrika Mashariki katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mikutano ya Mwaka ya Bodi ya Magavana (Mawaziri wa Fedha kutoka nchi wanachama) katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Nairobi, Kenya. Katika Mikutano hiyo, Dkt. Mwamba amemwakilisha Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Magavana (Mawaziri wa Fedha kutoka nchi wanachama) wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), baada ya Mkutano wa kawaida wa Magavana kutoka Kundi la Nchi za Afrika Mashariki ambao ni wanachama wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ikiwa ni maandalizi ya Mikutano ya Mwaka 2024 ya Bodi ya Magavana (Mawaziri wa Fedha kutoka nchi wanachama) inayofanyika Jijini Nairobi nchini Kenya. Katika Mikutano hiyo, Dkt. Mwamba amemwakilisha Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba. 
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Magavana (Mawaziri wa Fedha kutoka nchi wanachama) katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na wawakilishi wao, baada ya Mkutano wa kawaida wa Magavana kutoka Kundi la Nchi za Afrika Mashariki ambao ni wanachama wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ikiwa ni maandalizi ya Mikutano ya Mwaka 2024 ya Bodi ya Magavana (Mawaziri wa Fedha kutoka nchi wanachama) inayofanyika Jijini Nairobi nchini Kenya. Katika Mikutano hiyo, Dkt. Mwamba amemwakilisha Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.