Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia TAZARA ni kampuni ambayo inafanya usafirishaji wa mzigo kupitia mpaka wa Tunduma mkoani Songwe ambapo Zambia na DRC Congo ndiyo zenye kutumia kwa kiwango kikubwa reli ya Tanzania kwa kubeba mzigo yake mingi kutoka bandari ya Dar es Salaam.

Hayo yameelezwa na Fuad Abdallah Meneja Mkuu wa TAZARA upande wa Tanzania wakati akizungumza na waandishi wa habari waliofika katika banda la TAZARA leo kwenye maonesho ya Nanenane 2022 yanayofanyika kwennye viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya.

Amesema takwimu zinaonyesha teluthi moja ya mzigo wote unaosafirishwa kutoka bandari Dar es Salaam unakwenda Zambia, Congo DRC na nchi zingine zilizozunguka Tanzania ukizingatia kwamba katika nchi kama 6 ambazo Tanzania inapakana nazo zipo zaidi ambazo zinaweza kutumia fursa ya reli ya TAZARA.

Zambia na Congo peke yake zinaweza kusafirisha mzigo wa tani milioni 6 ambao ni mkubwa sana na injini zetu na mabehewa yetu yana ukomo fulani wa kubeba mzigo hivyo ni muhimu mkajenga reli mkawa na miundombinu ya reli lakini katika usafirishaji wa mizigo mkaingia ubia na makampuni mengine binafsi ambayo yatabeba mizigo pia.

Maelekezo ya mwanzo ya kuhusu sekta binafsi kusafirisha mizigo kupitia reli ya TAZARA yalitolewa katika kikao cha marais wawili Mh. Jakaya Kikwete Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa wakati huo na Rais wa Jamhuri ya Zambia Mh. Edger Lungu kwa wakati huo ambapo walifanya kikao jijini Lusaka Zambia na kuiagiza Tazara kuanza mchakato wa kuingia ubia na makampuni binafsi kutumia rei ya Tazara hivyo bodi ya wakurugenzi ya Tazara inafanya haya ili kutekeleza maagizo yaliyotolewa na marais hao

Hivi sasa kuna injini zetu na mabehewa lakini yana ukomo wa kubeba mzigo na ukiangalia maendeleo ya kisasa ya usafirishaji ni kwamba unaweza kujenga reli lakini pamoja na injini zako na mabehewa ukaingia ubia na makampuni binafsi ambayo yataingiza treni zake na kusafirishi mizigo kwa kutumia miundombinu yako hivyo ukaboresha huduma zako za usafrishaji jambo ambalo hata sisi TAZARA tumeshaanza kulifanya

Kwa sasa tumeingia mikataba na makampuni matatu ya usafirishaji mizigo kutoka Afrika Kusini ambayo injini zake na mabehewa yanatumia miundombinu yetu kusafirisha mizigo jambo ambalo pia limeongeza ajira kwa wananchi wetu kwani injini hizi zinaendeshwa na watanzania lakini pia baadhi ya wafanyakazi ni watanzania hivyo kuongeza ajira kwa watanzania

By Jamhuri