Mhandisi Aivan Maganza ambaye ni Mwenyekiti wa Vijana wa Chama Cha Tanzania Labour Party  (TLP), amesema kuwa uchaguzi wa nafasi ya mwenyekiti chama hicho ngazi ya taifa utafanyika Juni 18, 2023. 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini katika Makao Makuu ya TLP Magomeni jijini Dar es Salaam Maganza amesema kuwa hayo ni makubaliano yaliyofikiwa na Halmashauri Kau ya chama hicho.

“Viongozi wote wa Makao Makuu, ambao namanisha wa vitengo vya vijana, akina mama pamoja na wazee na mkutano mkuu Halmashauri kuu katika azimio lake la Machi 5, 2023, tulikubaliana kwamba uchaguzi mkuu TLP nafasi ya Mwenyekiti ufanyike Juni 18 Mwaka huu” amesema.

“Tumekubaliana kwa pamoja mkutano mkuu wa TLP Taifa wa kumchagua Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party utafanyika Juni 18, 2023, hivyo taarifa iwafikie wajumbe wa mkutano mkuu TLP Taifa popote walipo kwamba chama makao makuu kwa kushirikiana na idara tutaandaa utaratibu wote, na tayari maandalizi yapo tayari kwamba tutakutana kwa ajili ya uchaguzi.

Pia Mhandisi Maganza amewajulisha wagombea wote wajiandae kwa ajili ya uchaguzi huo.

By Jamhuri