Na Mary Margwe, JamhuriMedia, Kaliua

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora Grace Quintine amesema wamefanya Kikao cha Ujirani mwema na Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua ili kupitia upya mipaka ya Kiutawala kati ya Wilaya ya Urambo na Kaliua kwa Maslahi mapana ya Wananchi ili kurahisisha huduma kikamilifu.

Quintine amesema kikao hiko kimehusisha kuwakutanisha viongozi mbalimbali wa Wilaya zote mbili wakiwemo wakulu wa Wilaya wakurugenzi pamoja na wataalam mbalimbali wakiwemo wa ardhi wa pande hizo mbili kwa lengo la kuweka usawa wa jambo hilo ili jamii iweze kuondokana na hali ya sintofahamu.

Amesema wakiwemo katika kikao hiko wamefanikiwa kujadili mambo muhimu kama ustawi wa Jamii kwani Wilaya ya Urambo na Kaliua ni majirani , hivyo basi wananchi wa Wilaya hizo mbili hushirikiana katika shughuli mbalimbali kama za kiuchumi ikiwepo biashara.

“Tumekutana hapa Kaliua kwa lengo moja la kuadili Mambo muhimu ikiwemo Ustawi wa Jamii kwani Wilaya ya Urambo na Kaliua ni Majirani hivyo basi Wananchi wa Wilaya hizi Mbili hushirikiana katika Shughuli za Kiuchumi ikiwemo biashara” amesema Mkurugenzi Mtendaji Grace

Aidha Quintine amesema kikao hiko kimeleta manufaa makubwa na kukubaliana kwamba Wataalamu wetu wa Idara ya Ardhi kushirikiana kupitia upya maeneo yetu ya Kiutawala hasa tunapoeleke kwenye Chaguzi Mbalimbali ikiwa ni pamoja na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na uchaguzi Mkuu 2025.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo amezishukuru Kamati za Ulinzi na Usalama zote mbili chini ya Wakuu wa Wilaya akiwepo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Elibariki Bajuta Mkuu wa Wilaya ya Urambo na Dkt. Rashid Chuachua Mkuu wa Wilaya ya Kaliua kwa kusimamia vyema kikao hiko huku wakiwemo Viongozi wengine mbalimbali kwa Ushirikiano mwema kuwahudumia Watanzania kwa ufanisi mkubwa.

” Binafsi nizishukuru Kamati zote mbili za Ulinzi na Usalama za Wilaya zetu chini Wakuu wa Wilaya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Elibariki Bajuta Mkuu wa Wilaya ya Urambo na Dkt. Rashid Chuachua Mkuu wa Wilaya ya Kaliua kwa kusimamia vyema kikao chetu kimeenda vizuri na Viongozi wenzangu kwa Ushirikiano mwema kuwahudumia Watanzania kikamilifu ” amefafanua Quintine.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo amemshukuru Mh.Rias Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna ya kipekee ya kuendelea kuwapatia Miradi Mbalimbali ya Maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Urambo na Kaliua