Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga amesema katika Jimbo la Singida Kaskazini Vijiji 6 vimesalia kuunganishwa na umeme kati ya vijiji 84 vya jimbo hilo.

Amesema hayo wakati akisalimia wananchi katika Kijiji cha Sagara, wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani Singida iliyoanza leo tarehe 15 Oktoba, 2023.

Kapinga amesema Vijiji vyote nchini ambavyo havina umeme vitapata umeme kupitia miradi mbalimbali ya usambazaji umeme vijijini inayoendelea ukiwemo mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu mzunguko pili.