Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Robert Masunya na naibu mkurugenzi wa Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Malaki Msigwa wakimkabidhi hati ya kimila mmoja ya wananchi wa kijiji cha Mlanda ambaye ni mlemavu 
Naibu mkurugenzi wa Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Malaki Msigwa akitoa neo kwa wananchi wa kijiji cha Mlanda wakati wa kutoa hati za kimila 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Robert Masunya na naibu mkurugenzi wa Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Malaki Msigwa wakimkabidhi hati ya kimila mmoja ya wananchi wa kijiji cha Mlanda ambaye alikuwa anawakilisha kundi la wazee
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kushirikia zoezi la utoaji wa hati miliki za kimila zilizotolewa na Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID)
Picha ya pamoja baina ya viongozi wa Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID),viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Iringa pamoja na baadhi ya wananchi walikuwa tayari wamepokea hati za kimila
 
JUMLA ya wanakijiji 772 kati ya 1890 wa kijiji cha Mlanda kata ya Magulilwa wilaya ya Iringa mkoani Iringa wamepimiwa maeneo na mashamba yao na kukukabidhiwa hati miliki za kimila zinazotolewa kupitia Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID).
Hati hizo zilikabidhiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Robert Masunya wakati wa sherehe fupi za kuwakabidhi hati hizo zilizofanyika kijijini hapo na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi na wageni mbalimbali walikuwepo katika tukio hilo.
Akizungumza na wanakijiji hao baada ya kukabidhi hati hizo Masunya alisema kuwa hati hizo zitawasaidia kutenga maeneo kwa ajili ya matumizi mbalimbali kwa kuzingatia uwezo wa ardhi kuhimili idadi hiyo na kasi ya ongezeko la watu na mifugo kwa miaka mingi ijayo.
Masunya aliongezea kuwa,hatua hiyo itasaidia kupunguza migogoro ya ardhi kwa kuimarisha usalama wa miliki za ardhi na kuongeza thamani ambayo itawawezesha hata kukopesheka katika taasisi za kifedha zikiwemo benki.“Usajili wa ardhi ni muhimu kwasababu unaongeza ulinzi wa umiliki wa ardhi, unawezesha uwekezaji, unaongeza thamani ya ardhi na unapunguza migogoro ya ardhi,” alisema Masunya
Masunya aliupongeza mpango huo akisema utasaidia kupunguza eneo kubwa la ardhi ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ambayo haijapimwa.
Aidha Masunya aliwaomba Feed The Future wautanue mradi huo angalau ufike umalize kupima vijiji vyote vya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa huku akivikumbusha vijiji vyote vya wilaya hiyo kuendelea kutoa ushirikiano kwenye miradi ambayo inasaidia kukuza maendeleo ya nchi.
“Tunataka katika kipindi ambacho Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) tuhakikishe tunapima ardhi na mipango ya matumizi bora na ipimwe ili kila mwenye kipande chake cha ardhi awe na hati yake,” alisema Masunya.
Alisema kwa kupitia sera hiyo, kutakuwa na usimamizi zaidi wa ulinzi wa ardhi ya watu masikini ili kupunguza uporaji wa rasilimali hiyo unaofanywa na matajiri.“Marekebisho ya sera hiyo ya ardhi yatawezesha pia kufanyika kwa mrekebisho ya sheria mbalimbali za ardhi ili ziendane na sera na mazingira ya sasa,” alisema Masunya.
Masunya aliwataka wanakijiji wa kijiji hicho ambao hawajapimiwa maeneo yao kwa sababu mbalimbali ikiwemo ubishi na migogoro ya kifamilia kutumia vizuri muda ambao bado mradi huo upo katika wilaya hiyo na kuhakikisha nao wananufaika na zoezi hilo.
Wanakijiji ambao hawajapimiwa maeneo yao wanaweza kuendeleoa kuzalisha migogoro ambayo haina tija kwa maendeleo yao na kusababisha waendelee kuwa masikini kwa kuwa hawatakuwa na dhamana ya kwenda kukopa.
Awali naibu mkurugenzi wa Mradi wa LTA, Malaki Msigwa alisema kuwa kijiji cha Mlanda kinajumla ya wananchi 1890 na walio nufaika na Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) ni wananchi 772 na kufanikiwa kutoa jumla ya hati miliki za kimila 1777 ambapo wanaume walikuwa 409 na wanawake 363.
Msigwa aliwapongeza wataalamu wa mradi huo kwa kuhakikisha wanawasaidia wananchi wa kijiji cha Mlanda kupima maeneo yao na kupata hati miliki za kimila ambazo zitakuwa msaada mkubwa kwenye maendeleo ya kiuchumi.
“Baadhi ya miradi imeibuliwa wakati wa upimaji wa ardhi hivyo ni fursa sasa kwa wananchi wenyewe kuitumia vizuri ardhi waliyopimiwa na kupewa hati miliki za kimila na kwa kuwa asilimia fulani kijiji hiki kimepimwa hivyo wanaweza kuwa kijiji cha mfano kwa kuwapa maendeleo hata wawekezaji wazuri kwa faida yao” alisema Msigwa
Msigwa alisema kati ya vijiji hivyo 41 vitakavyotayarishiwa mipango ya matumizi bora ya ardhi na kila mwenye ardhi kupimiwa na kupewa hati miliki za kimila, vijiji 36 vipo wilayani Iringa na vitano vipo wilayani Mbeya.
“Baada ya kukamilisha zoezi la upimaji mashamba na urasimishaji wa kijiji chote cha Mlanda, hivi sasa mradi unaendelea na upimaji mashamba katika vijiji vya mradi ambavyo vipo wilayani Iringa” alisema Msigwa
Naye diwani wa kata ya Magulilwa Jane Mhangala aliupongeza Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) kwa kuzingatia jinsia wakati walipokuwa wanaendesha zoezi la upimaji ardhi katika kijiji hicho.
“Hongera sana LTA kwa kuwapa elimu wanawake na wanaume na kuhakikisha kuwa wanapa haki zao sawa bila kuwa na mgogoro wowote tofauti na ilivyokuwa hapo awali,maana miaka ya nyuma mwanamke alikuwa anabaguliwa kwenye kila kitu wala alikuwa haruhusiwi hata kumili ardhi” alisema Mhangala.Mhangala aliongeza kwa kusema kuwa wanakijiji wa kijiji cha Mlanda baada ya kupata elimu ya kumiliki ardhi kumepunguza sana migogoro ambayo ilikuwa inaleta chuki kwenye familia.
“Kwa sasa ardhi ya kijiji hiki imepanda dhamani kwa kiasi kikubwa na tayari ishapimwa na mmepata hati miliki za kimila ambazo zitawasaidia katika maendeleo yenu ya kiuchumi” alisema Mhangala

By Jamhuri