Na Cresensia Kapinga, JamhuriMedia, Songea
Mkuu wa Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Kapenjama Ndile amewataka Wmqafanyabiashara na wananchi kutumia nishati safi ya kupikia ikiwemo gesi ili kutunza mazingira na kuokoa misitu inayoteketea kutokana na matumizi makubwa ya Kuni na mkaa.
Ndile ameyasema leo wakati akifungua kikao cha wadau wa mafuta Songea kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa Songea mkoani Ruvuma ambapo kikao hicho kimeandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji (EWURA) kanda ya nyanda za juu kusini.

Alisema kuwa kipekee Rais Dk Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza kusimamia swala la utekelezaji wa mkakati wa Kitaifa juu ya matumizi ya Nishati safi ya kupikia lengo likiwa ni kukabiliana na mabadiliko ya tabia Nchi na si vinginevyo.
Kwa upande wake Meneja wa Kanda za Nyanda za juu kusini Karim Ally alisema kuwa lengo la kikao hicho ni kutaka kufikisha huduma Bora ya Nishati katika maeneo ya vijijini ambako bado kulikuwa na changamoto ya utumiaji wa nishati hiyo.
Nao wadau wa kikao hicho wamepongeza EWURA kwa kuandaa kikao hicho na kwamba wataenda kutoa huduma bora kwenye maeneo ya vijijini ili kupunguza adha iliyokuwa ikiwakabili Wananchi waishio Vijijini kuhusu Nishati.

