Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia,
Kampuni ya Chem Chem Safari ya Tanzania imeingia katika ushirikiano na Auberge Collection chini ya chapa ya Auberge Safari.
Ushirikiano huu umejengwa juu ya dhamira ya pamoja ya kutoa huduma zinazozingatia mazingira ya eneo husika, zilizoandaliwa mahsusi na zikizingizatia urithi, utamaduni wa maeneo, na uhusiano na mazingira hayo.
Uidhinishaji wa Auberge unaongeza alama inayotambulika ya ubora wa kitaalamu wa bidhaa ambayo imeheshimika kwa muda mrefu katika soko maalum la wateja.
Ikiwa kati ya Ziwa Manyara na Hifadhi ya Taifa ya Tarangire, Chem Chem ni chimbuko la falsafa ya “Slow Safari” mtazamo mpya wa uzoefu wa safari unaojengwa juu ya uzoefu wa makusudi, uwepo wa kweli, na uhusiano wa kina zaidi na mazingira ya asili.
Kila moja ya kambi zake tatu ina sifa ya kipekee ambapo Chem Chem Lodge kama sehemu ya mapumziko ya kifahari na tulivu; Little Chem Chem ikiibua ukaribu wa kambi ya mtindo wa wachunguzi (explorer-style) na Forest Chem Chem ikitoa faragha na uzoefu wa kutulia ndani ya mazingira ya msitu tulivu.
Kupitia Chama cha Chem Chem, kampuni inasaidia kulinda Korido/Njia ya Wanyamapori ya Kwakuchinja, ambayo ni njia muhimu ya uhamaji wa wanyama inayounganisha Tarangire na Ziwa Manyara, pamoja na kuendesha programu za maendeleo ya jamii kwa muda mrefu.
Muhimu zaidi, ushirikiano wa Auberge Safari unaimarisha maono haya huku umiliki wa kampuni na dhamira zake za uhifadhi zikiendelea kubaki bila mabadiliko.
Chem, kampuni inasaidia kulinda Korido/Njia ya Wanyamapori ya Kwakuchinja, ambayo ni njia muhimu ya uhamaji wa wanyama inayounganisha Tarangire na Ziwa Manyara, pamoja na kuendesha programu za maendeleo ya jamii kwa muda mrefu.
Muhimu zaidi, ushirikiano wa Auberge Safari unaimarisha maono haya huku umiliki wa kampuni na dhamira zake za uhifadhi zikiendelea kubaki bila mabadiliko.


