….Mmoja apungua kutoka kilo 148 mpaka kilo 108
Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam
HOSPITALI ya Shifaa ya Kinondoni Dar es Salaam imewafanyia upasuaji wa kupunguza uzito ambao umekuwa wa wenye mafanikio kwa kutumia tundu dogo watu 20 waliokuwa na uzito mkubwa.
Akizungumza hospitalini hapo jana, Daktari bingwa wa upasuaji wa hospitali hiyo, Murad Tarmohamed, alisema hospitali hiyo imeweka wataalamu bobezi kwa ajili ya taaluma hiyo.
“Watu wengi wanadhani kuwa upasuaji huu ni kwaajili ya urembo hapana, unafaida nyingi sana kama kuepuka magonjwa ya sukari na wakishafanyiwa wakapona kabisa, kuna watu wanakosa pumzi sababu ya uzito mkubwa wakifanyiwa wanapona,” alisema
Alisema kuna watu ambao wanapata shida ya magoti na nyonga sababu ya maumivu wanayopata wanapotembea lakini wakifanyiwa upasuaji wanapona.
Alisema magonjwa kama ya moyo yanayotokana na uzito kuwa mkubwa yamekuwa yakiondoka kwa watu wanaofanyiwa huduma hiyo.
“Mtu anapofanyiwa upasuaji huu anakuwa na nguvu zaidi anarudi kwenye maisha ya kawaida, anaacha kuchoka mara kwa mara anakuwa anafanya shughuli zake kama zamani, tunasisitiza ni muhimu sana si kwa muonekano bali kwa ajili ya afya ya mhusika,” alisema
“Umuhimu wa upasuaji kama huu ni shida ambazo unaondokana nazo baaada ya upasuaji kama moyo, sukari, presha sukari, maumivu ya nyonga, magoti na kukosa pumzi ukiwa umelala,” alisema hiyo ni kambi ya tatu kufanya hospitali ya Shifaa
“Faida ya upasuaji huu ni kwamba mgonjwa hakai sana hospitalini, akifanyiwa leo kesho anatoka anakwenda nyumbani kuendelea na maisha yake kama kawaida,” alisema
Shuhuda mmoja aliyefanyiwa upasuaji huo, Bashir Haroon alisema alikuwa ana kilo 140 lakini baada ya upasuaji uzito wake umeshuka hadi kufikia kilo 90.
“Mimi nilikuwa na kilo 140 na nilikuwa Napata shida sana katika maisha ya kila siku ndiyo sababu nilileta wataalamu bingwa kutoka nje ya nchi kuja kusaidiana na mabingwa wetu kufanya upasuaji wa aina hii,” alisema Haroon ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya Shifaa
“Tunapofanyakambi kama hizi tunataka kutoa huduma bora kwa watanzania kwa kutumia wataalamu wetu bingwa wa hapa nchini na upasuaji umekuwa wa mafanikio makubwa sana,” alisema
Haroon huduma hiyo imekuwa msaada mkubwa sana kuokoa wananchi kupata maradhi mbalimbali kama ya moyo, sukari, figo na kuwa na afya jema.
Shuhududa mwingine, Hassan Sharman alisema kabla ya upasuaji huo alikuwa na shida sana ya shinikizola damu lakini baada ya upasuaji ameondokana na tatizo hilo.
Alisema awali alikuwa na uzito wa kilo 148 lakini baada ya upasuaji huo amefanikiwa kupungua hadi kufikia kilo 104 hivyo kupunguza kilo 40.
“Nilikuwa nafanya mazoezi sana lakini sipungui ndipo nilipoona tangazo kwamba hospitali ya Shifaa wanatoa huduma hii. Ni upasuaji salama sana hauna shida yoyote ile, natembea kilomita hadi 10 kwa siku sina shida kama zamani,” alisema
“Kuna watu wanadhani ukifanya upasuaji kama huu unapata shida ya kiafya lakini si kweli, upasuaji huu unakuondoa kwenye maradhi kama ya shinikizo la damu, sukari na mengine mengi tu,” alisema



