Author Archives: Jamhuri

Most Noticeable Dating Online

Dating Online Secrets That Nobody Else Knows About Teaming up with a person on the world wide web is alright but you have to be truthful regarding the reason. As talking on the web is the principal sort of communication it is perfectly alright to send an email to this person who has the copy motives. When you talk to ...

Read More »

the Brand New Angle On Fun Just Released

Afternoon snacks will be furnished throughout the week. Simply speaking, it felt the same as being a recipe for a amazing party full of fun wedding thoughts. Sure, some folks just have lousy taste. In order have the ability to inspire individuals who create stuff, HBS students will require to understand to empathize with people who do it now. Making ...

Read More »

‘Balozi’ Alphayo Kidata kufikishwa mahakamani

Kuna kila dalili kuwa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada, Alphayo Kidata, atafikisha mahakamani Kisutu muda wowote kuanzia sasa kujibu tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka wakati akiwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), uchunguzi wa JAMHURI umebaini. Kidata aliapishwa Mei 10, mwaka huu kwenda kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada, alikokwenda kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Balozi ...

Read More »

Mchati: Mti wa thamani unaotoweka Mafia

Licha ya ukweli kuwa uoto wa asili wa Kisiwa cha Mafia unafanana kwa kiasi kikubwa na uoto wa asili wa visiwa jirani vya Pemba na Unguja na maeneo ya Bara yaliyopo jirani kama Kisiju na Rufiji, watafiti Rogers na Greenaway (1988) waliokuwa wakidurusu uoto wa Kisiwa cha Mafia walishangazwa mno na kiwango kikubwa cha upekee (endemism) wa mimea ya kisiwa ...

Read More »

Benki Kuu yaichunguza BOA

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeanza kuichunguza Benki ya BOA ambayo Gazeti la JAMHURI limeandika kwa wiki mbili mfululizo kuelezea jinsi inavyochezea dhamana za wateja, JAMHURI limeelezwa. Wateja wengi wa BOA wamejitokeza na malalamiko ya aina mbalimbali dhidi ya benki hii yenye kuonyesha ukiukwaji mkubwa wa Sheria ya Benki na Maduka ya Fedha ya Mwaka 2006, ikiwamo kuwaongezea wateja riba ...

Read More »

Amri ya DC Moshi yamchefua Askofu, wananchi Vunjo

Askofu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini, Dk. Martin Shao, amepinga amri ya Mkuu wa Wilaya (DC) ya Moshi, Kippi Warioba, kuzuia ujenzi wa barabara vijijini katika Jimbo la Vunjo. Barabara hizo zinajengwa kwa nguvu za wananchi kwa kushirikiana na Taasisi ya Maendeleo Vunjo (VDF). Askofu Shao ambaye ni Mwenyekiti wa VDF, amewambia waandishi ...

Read More »

Makamu wa Rais: Ole wenu wavamia hifadhi

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, ametoa onyo kwa wananchi wenye tabia ya kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya maeneo ya hifadhi, akiwataka waache mara moja na wale watakaoendelea wasije kuilaumu serikali kwa hatua itakazochukua dhidi yao. Ameyasema hayo wakati akizindua rasmi Jeshi Usu ambalo limepewa jukumu la kulinda maliasili za nchi, ikiwemo wanyamapori na misitu, Fort Ikoma, Serengeti mkoani ...

Read More »

Uonevu kwa wakulima ufikie tamati

Tunapongeza hatua iliyochukuliwa na serikali kwa wakulima wa korosho. Japo matokeo ya uamuzi huo hayajajulikana, lililo la msingi ni kuwa serikali imeonyesha kuwajali wananchi hao. Historia inaonyesha kuwa kwa miongo mingi wakulima wa mazao ya aina zote wamekuwa wakidhulumiwa licha ya matamko mengi ya kuwatia moyo. Ufisadi mkubwa umekuwapo kwenye sekta hii kiasi cha kuwafanya wakulima wengi waishi na hatimaye ...

Read More »

Inawezekana kufanyika, fanya sehemu yako

Miongoni mwa maneno muhimu na ninayoyakubali kwa asilimia mia yaliyowahi kusemwa na Mwalimu Julius K. Nyerere, ni haya: “Inawezekana kufanyika, timiza wajibu wako.” Tumezoea kusikia watu wengi wakilalamika; na ngao kubwa ya kutofanya mambo makubwa huwa wanajikinga na ngao ya umaskini. Utasikia wakisema: “Kwetu tulikuwa maskini wa kutupwa, wazazi wangu hawakuweza kumudu kununua hiki na kile.” Muda mwingine utasikia wakilalamikia ...

Read More »

Kesi ya Jaji Warioba, TBA kusikilizwa mwakani

Kesi iliyofunguliwa na Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais mstaafu, Jaji Joseph Warioba, dhidi ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), imeahirishwa hadi Februari 11, mwakani. Jaji Warioba ambaye pia amewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, anapinga kufukuzwa katika nyumba Na. 501/13 iliyopo Barabara ya Ghuba, Oysterbay jijini Dar es Salaam kutokana na mgogoro wa kodi ya pango. Kesi ...

Read More »

Maajabu ya Ngorongoro

Hifadhi ya Ngorongoro (NCA) ina eneo la ukubwa wa kilometa 8,300 za mraba – lenye mchanganyiko wa pekee wa sura ya nchi, wanyamapori, wanyama wafugwao na mambo ya kale. Hifadhi hii ilianzishwa mwaka 1959 chini ya Kifungu cha Sheria Na. 413 kuwa eneo lenye kuhifadhi maliasili, kulinda mila na kuendeleza masilahi ya wenyeji wafugaji waishio ndani ya eneo, pia kukuza ...

Read More »

Raila Odinga anakuwa Rais Kenya (7)

Wiki iliyopita makala hii iliishia katika aya iliyosema: “Mkakati wake [Raila Odinga] kuitisha kura za maoni kubadilisha Katiba nadhani umefikia tamati. Asante rais kwa kutia mkono wako katika uteuzi wa Odinga na kumshawishi akaukubali,” anasema Mbunge wa Kiharu, Ndindi Nyoro.” Je, unafahamu kuwa kabla ya uteuzi huu Odinga alikataa uteuzi mara kadhaa? Endelea… Odinga aliwahi kuukataa Ubalozi Maalumu wa Umoja ...

Read More »

Sababu za kutosikia kwa ufasaha

Mawimbi ya sauti yanaingia kwenye sikio la nje kupitia mfereji wa sikio; hivyo kusababisha ngoma ya sikio na ile mifupa midogo midogo milaini sana ndani ya sikio inayojulikana kama ngoma ya sikio iliyopo katika sikio la kati kutetemeka. Kutetemeka kwa ngoma ya sikio kunaruhusu mitetemo hii ya sauti isafiri hadi kwenye sehemu inayoitwa ‘koklia’. Koklia inapokea mawimbi ya sauti  na ...

Read More »

‘If you can’t fight them, join them’ (2)

Sehemu iliyopita mwandishi wa makala hii alirejea hadithi iliyotolewa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kuhusu msichana mzuri aliyekuwa akichumbiwa. Akaeleza namna Mwalimu alivyohakikisha hageuki jiwe katika kuijenga nchi kwenye misingi ya kijamaa. Hii ni sehemu ya pili na ya mwisho ya makala hii. Endelea… Basi, kwa ustaarabu wa wenzetu kule ‘majuu’, mtu unaposhindwa katika uchaguzi unakubali matokeo ...

Read More »

Tuwe waangalifu kilimo kimejaa hadaa, hujuma

Historia duniani inaonyesha jinsi ambavyo mbinu mbalimbali zimetumika kudidimiza kilimo katika nchi zetu ili tugeuke wategemezi. Hujuma ya kwanza dhidi ya kilimo chetu ilikuwa enzi ya ukoloni. Wakoloni hawakutaka tujitosheleze kwa chakula au tuanzishe viwanda vinavyotumia mazao ya kilimo. Enzi ya ukoloni tulilazimishwa kulima mazao yanayokidhi mahitaji ya viwanda vya wenzetu. Ikawa piga ua lazima tulimishwe katani, chai, pamba na ...

Read More »

Kazi si balaa, kazi ni baraka 

Binadamu anaposhirikiana na binadamu wenzake katika kufanya kazi huwa hana budi kutimiza mambo matatu; wajibu, uwezo na kujituma. Anapotimiza haya hupata maendeleo yake na ya wenzake.  Hii ni moja ya taratibu za binadamu katika kufanya kazi. Watanzania hatuko nje ya utaratibu huu. Lakini baadhi yetu hatufuati mambo haya kwa sababu tunadhani au tunaamini kazi ni balaa, kazi ni utumwa, ilhali kazi ni ...

Read More »

Yah: Adha ya mlalahoi wa Kitanzania

Nichukue fursa hii kutoa salamu zangu za dhati kwa mtu ambaye alikuwa akijulikana kwa jina la mlalahoi miaka michache baada ya kuingia mfumo wa vyama vingi vya siasa hapa nchini. Jina hili tulipewa kundi fulani na wanasiasa wetu kwa lengo la kutuonyesha tofauti tuliyonayo sisi na baadhi ya wafanyabiashara au wafanyakazi wakati huo. Walalahoi tulijijua bila hata kuuliza, kwa maana ...

Read More »

Ndugu Rais njia yetu ni moja

Ndugu Rais, imeandikwa kuwa mwanadamu ni mavumbi. Mavumbini ulitoka na mavumbini utarudi! Ulitoka kwa udongo na utarudi kwa udongo! Kati yetu sisi wote hakuna atakayekufa halafu jeneza lake lihifadhiwe dalini au juu ya mti kama mzinga wa nyuki. Haijalishi litakuwa na thamani ya kiasi gani na wala haijalishi kama litafunikwa sanda ya bendera ya taifa au kaniki. Jeneza letu litafukiwa ...

Read More »

DAWASA yaongeza mapato

Rais Dk. John Magufuli ametimiza miaka mitatu madarakani. Katika kipindi hiki taasisi kadhaa za serikali zimekuwa zikielezea mafanikio yaliyopatikana katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Katika kutekeleza azima ya kuelezea kuhusu mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA), Mhandisi Cyprian Luhemeja, amesema mamlaka ...

Read More »

Haki za watoto hazilindwi inavyostahili

Leo ni Siku ya Kimataifa ya Watoto. Kihistoria ni siku iliyoanza kuadhimishwa tangu karne ya 18, lakini sasa inatambuliwa rasmi na Umoja wa Mataifa. Ni siku inayopewa jina la watoto, lakini ukweli ni siku ya watu wazima kutafakari iwapo wanasimamia vyema jukumu lao la kulinda haki na maslahi ya watoto. Katika hotuba aliyotoa Ikulu mwaka 1964 ikiwa imelengwa kwa watoto, ...

Read More »

Sheria inapomtambua mvamizi wa ardhi

Ni muhimu kutahadharishana kuhusu jambo hili. Kitaalamu jambo hili huitwa ‘adverse possession.’ Ni kanuni ya kisheria. Ni wakati ambapo mtu au watu wanavamia ardhi yako, lakini baada ya muda wanahesabika kuwa ni wamiliki halali. Na wanatambuliwa hivyo na sheria na wewe mmiliki halisi unageuka kuwa mvamizi. Lakini hoja kubwa hapa si lazima mtu awe mvamizi. Anaweza kuwa mpangaji au mtu ...

Read More »

MAISHA NI MTIHANI (4)

Malezi ya watoto ni mtihani. Maisha ya mtoto ni kama karatasi nyeupe ambapo kila mpita njia anaacha alama. Kwa msingi huo malezi ya watoto ni mtihani, maana kila mpita njia anaweza kuacha alama hasi au alama chanya. Kusema kweli anayetoka kipindi cha utoto anastahili pongezi. Socrates – mwanafalsafa wa Ugiriki aliwaambia watu wa Athens: “Kwa nini mnasugua kila jiwe (kila ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons