Nyundo ya Wiki

Sijasikia ACCACIA wakijitetea, namsikia Mtanzania Tundu Lissu akiwatetea!

Sijasikia ACACIA wakijitetea, bali namsikia Mtanzania mwenzetu Tundu Lissu katika maandishi na video zinazoenezwa mtandaoni kwa kasi ya ajabu akiwatetea kwa nguvu na kwa pumzi zake zote. Ni kuhusu mchanga wenye madini uliozuiwa na Serikali bandarini. Amezungumzia mambo ambayo nitayajibu hapa kwa lengo kubwa kabisa la kutaka Watanzania wafahamu.   Je, sheria inasema mchanga ni mali ya ACACIA? Lissu anasema ...

Read More »

Utajiri Mhasibu Takukuru watisha

Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam, Kisutu, imetoa amri ya zuio la mali za Mhasibu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Godfrey Gugai. Amri ya Mahakama ya Kisutu ilitolewa Mei 8, mwaka huu; na Gugai anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya rushwa na mengine kulingana na tuhuma zinazomkabili. Kuzuiwa kwa mali hizo kumetokana na maombi yaliyowasilishwa ...

Read More »

Ugaidi waifilisi Benki FBME

Kufungwa kwa benki ya FBME, hapa nchini, kumetokana na tuhuma za benki hiyo kutakatisha fedha na kupitisha fedha za kufadhili ugaidi ambazo zimekuwa zikipitishiwa kwenye matawi yake ya Nicosia, Cyprus na Makao Makuu ya benki hiyo, Dar es Salaam, JAMHURI limebaini. Julai, 2014 Benki Kuu ya Cyprus, pamoja na Benki Kuu ya Tanzania, waliingilia kati na kuanza kuchunguza, uchunguzi huo ...

Read More »

Anne Makinda yamfika

Uamuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda, wa kuwafurusha wakurugenzi na watumishi kadhaa wa Mfuko huo, unaelekea kuitia Serikali hasara ya Sh bilioni 9. Kiasi hicho cha fedha huenda kikalipwa kwa watumishi hao ambao uchunguzi wa JAMHURI umebaini kuwa wamesimamishwa na wengine kufukuzwa kazi kinyume cha sheria. Muda mfupi baada ya ...

Read More »

‘Bureau de Change’ zafungwa Dar

Vyombo vya dola vimefunga maduka kadhaa ya kubadilishia fedha (Bureau de Change) jijini Dar es Salaam, yanayohusishwa na utakatishaji na usafirishaji fedha zinazotokana na biashara ya dawa za kulevya. Vyanzo vya habari vya uhakika vimelithibitishia JAMHURI kuwa tayari maduka matano yamefungwa kwenye operesheni hiyo inayohusisha Kikosi Kazi kinachoundwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Jeshi la ...

Read More »

Barabara yavunja rekodi

Wakati Rais John Magufuli, akijitahidi kubana matumizi, Manispaa ya Morogoro imejenga barabara ya lami yenye urefu wa Kilomita 4, kwa gharama ya Sh bilioni 12. Gharama hiyo imevunja rekodi ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami nchini, uchunguzi wa JAMHURI umebaini. Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) umekuwa ukijenga kilomita moja ya tabaka la lami nzito kwa gharama ya Sh ...

Read More »

Ukweli usemwe kutekwa kwa Roma Mkatoliki

Msanii wa Bongo Fleva, Ibrahim Musa aka Roma Mkatoliki, aliyetoweka baada ya kudaiwa kukamatwa mapema siku ya Alhamisi katika mji wa Dar es Salaam, amepatikana na amekuwa akihojiwa kwa saa kadhaa baada ya kupatikana. Taarifa zinasema Roma Mkatoliki alirudi kwake Jumamosi alfajiri, na baadaye kuelekea kituo cha Polisi cha Oysterbay, Dar es Salaam, ambako alifanyiwa mahojiano na baadaye kupelekwa Hospitali ...

Read More »

Kigogo Ushirika kizimbani utakatishaji fedha

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Kilimanjaro (KNCU), Maynard Swai, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Arusha na Arumeru, jijini Arusha akishitakiwa kwa kosa la utakatishaji wa fedha. Swai, ambaye pia ni mwenyekiti mstaafu wa Chama cha Wakulima Tanganyika (TFA), katika mashtaka hayo yumo pia ofisa wa benki  moja Jijini hapa, Salvatory Mwandu, na Jesca Joseph ambaye ni mtumishi ...

Read More »

Bodi ya Ununuzi na Ugavi yawafunda viongozi

Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) kwa kushirikiana na wakufunzi kutoka taasisi ya Uongozi,  Mafunzo ya Uongozi, kwa viongozi wa vyama vya wanafunzi wa vyuo kadhaa hapa nchini wanaosomea fani ya ununuzi na ugavi. Mafunzo hayo ya siku moja yamefanyika Dar es Salaam katika Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kwa kuwakutanisha viongozi wataalamu 35, wenye taaluma ya ...

Read More »

Siri mjane ‘aliyejilipua’

Swabaha Shosi, ambaye wiki iliyopita alimweleza Rais John Magufuli namna anavyosumbuliwa na vyombo vya utoaji haki, kwa sasa analindwa na vyombo vya ulinzi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais. “Kwa kweli nashukuru, nimepewa ulinzi, ninao,” amesema Swabaha alipozungumza kwa simu na JAMHURI. Tofauti na kile kinachosambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, Swabaha amesema kuwa ana haki zote za mirathi ...

Read More »

Kijiji chawapa Wazungu ekari 25,000

Kampuni ya AndBeyond ya Afrika Kusini, imeingia mkataba na uongozi wa Kijiji cha Ololosokwan, Ngorongoro mkoani Arusha unaoiwezesha kuhodhi ekari 25,000 za ardhi kwa ajili ya utalii wa picha. Malipo yote yanayofanywa na kampuni hiyo yanaishia mikononi mwa viongozi wa kijiji ambao wanasema fedha hizo wanazitumia kwa shughuli za maendeleo huku Serikali Kuu ikiwa haiambulii kitu. Pamoja na kuingia mkataba ...

Read More »

Ufisadi watikisa katika ngozi

Azma ya Rais John Pombe Magufuli kuelekea nchi ya viwanda huenda isitimie kutokana na genge ya walanguzi kutoka nje ya nchi kuikosesha Serikali mapato zaidi ya bilioni 25, uchunguzi wa JAMHURI umebaini. JAMHURI imebaini ufisadi wa kutisha unaodidimiza sekata ya ngozi nchini, kutokana na uwepo wa mtandao wa wafanyabiashara walanguzi wa ngozi ghafi kuzisafirisha nje ya nchi kinyume cha sheria. ...

Read More »

Watendaji Kilwa wachunguzwa

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi, ameiagiza Wilaya ya Kilwa kuunda timu itakayofanya uchunguzi ili kubaini watendaji waliosababisha kukwama kwa ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Kisongo, pamoja na ujenzi wa maabara ya Shule ya Sekondari Kata ya Lihimalyao.  Zambi ameyasema hayo baada ya kufanya ziara ya kikazi Januari 7 mwaka huu, katika Kata ya Lihimalyao na kubaini mambo ...

Read More »

Msaka majangili ateswa

Siku 12 baada ya kumwandikia barua nzito, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Peter Mtani, amekamatwa na kuteswa kwa siku saba mfululizo kabla ya kuachiwa wiki iliyopita bila masharti. Mtani  amekuwa afisa wanyamapori daraja la pili, kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kuanzia Julai 2008 hadi Novemba 2016. Katika barua yake aliyomwandikia, Dk Lauren Ndumbaro, ambayo ...

Read More »

Wafanyabiashara na TRA

493. MATATIZO YA UTARATIBU HUU NA MIANYA YA RUSHWA (i) Idara ya Upelelezi, Uzuiaji na Mashtaka Makao Makuu na Kitengo cha Ofisi za kanda kinawasaka wakwepa kodi, wafanyabiashara ya magendo na wanaolipa kodi ndogo, ikiwezekana kukamata mali zao na kuwafungulia mashtaka. Kwa wale wanaokamatwa mara nyingi wamekuwa wanakubali kufikia usuluhishi nje ya mahakama ambapo mtuhumiwa na Afisa Forodha wanafikia maelewano ...

Read More »

RIPOTI YA RUSHWA YA JAJI WARIOBA – 25

TRA ina mianya ya rushwa     474. Idara hizi hukusanya asilimia 70 – 73 ya mapato yote ya Serikali Kuu yanayotokana na kodi mbalimbali. Hali ya ukusanyaji kodi katika idara hizi kwa kipindi cha miaka mitano imeonyeshwa katika kiambatisho A.  475. Pamoja na ongezeko katika makusanyo ya kodi bado uwiano kati ya mapato na Pato la Taifa ni mdogo. ...

Read More »

RIPOTI YA RUSHWA YA JAJI WARIOBA – 24

Viongozi Z’bar wawajibishwe (a) ADUCO INT. B.V. Ushahidi unathibitishakuwepo kwa mizengwe katika kupatiwa kazi kampuni ya UDUCO INT. B.V. kwamba licha ya Waziri kukubaliana na Katibu Mkuu wa Wizara awali kuwa kutokana na zabuni za ADUCO kuwa juu zaidi ya wazabuni wote ilikuwa viguu yeye kusaidia,bado mkutano ulioongozwa na Katibu Mkuu ukapitisha pendekezo la kuwapa kazi hiyo kampuniya ADUCO INT. ...

Read More »

RIPOTI YA RUSHWA YA JAJI WARIOBA – 23

Kaula, Dk. Mlingwa, rushwa ‘iliwapofusha’   Zabuni hizo zilipokelewa na kufunguliwa katika ofisi za Halmashauri Kuu ya Zabuni tarehe 26 Juni, 1991 na baadaye kukabidhiwa Wizara ya Ujenzi kwa uchambuzi na tathmini. Zabuni zilifanyiwa uchambuzi na tathmini na wahandisi wa Wizara. Taarifa ya kamati hiyo ilipendekezwa kuwa “Package” Na. 9 ya barabara ya Pugu- Chanika- Mbagala itolewe kwa kampuni ya ...

Read More »

RIPOTI YA RUSHWA YA JAJI WARIOBA – 20

Makandarasi ni shida   SEHEMU YA PILI   KANDARASI ZA UJENZI 408. Wizara ya Ujenzi ni miongoni mwa Wizara zinazotumia fedha nyingi za Serikali. Kwa mfano, katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 1994/95 bajeti ya Wizara ya Ujenzi ilikuwa sawa na 4.32% ya bajeti ya Serikali na 20.25% ya bajeti ya maendeleo ya Wizara na Idara za Serikali.  Aidha, ...

Read More »

RIPOTI YA RUSHWA YA JAJI WARIOBA – 16

Mahakimu wanadharau majaji   344. Tume inapandekeza kwamba: i)      Mamlaka ya Mahakama ihakikishe kwamba juzuu za sheria zinapelekwa katika Mahakama zote, hasa za mahakimu, zikiwa zimefanyiwa marekebisho yote yaliyofanywa na Bunge. ii)     Utaratibu wa kutoa vitabu vyenye kesi zilizoamuliwa (Law reports) urudishwe na vitabu hivyo visambaze kwenye Mahakama zote nchini. iii)     Mamlaka ya Mahakama ichukue hatua ...

Read More »

RIPOTI YA RUSHWA YA JAJI WARIOBA – 15

Nidhamu mahakimu imeshuka   Mapendekezo Tume inapendekeza kama ifuatavyo:-  (i)Ajira ya makarani wa mahakama katika ngazi zote ifanywe baada ya tathmini ya tabia ya waombaji kufanywa na idara. Kila inapowezekana idara itumie vyombo vingine vya taifa kupata taarifa za waombaji wa kazi hiyo;  (ii)Idara ibuni mpango wa kudumu wa elimu ya kujiendeleza kwa makarani wa mahakama kwa kanuni na taratibu ...

Read More »

RIPOTI YA RUSHWA YA JAJI WARIOBA – 13

Uhamiaji, mahakimu rushwa tu Mianya ya rushwa 282.  Mianya ya rushwa katika Idara ya Uhamiaji inatokana na baadhi ya vifungu vilivyomo katika Sheria ya Uhamiaji. Lakini sehemu kubwa ya mianya ya rushwa ni matokeo ya usimamizi wa kazi usioridhisha wa watumishi wa idara hiyo na kupuuzwa kwa umuhimu wake katika utaratibu mzima wa uendeshaji wa serikali. Kupuuzwa huko kumesababisha uongozi ...

Read More »
Show Buttons
Hide Buttons