




Mkuu wa Mkoa wa Kagera Albert Chalamila ametaja marehemu kuwa ni pamoja na Neema Faraja, Hanifa Hamza, Aneth Kaaya, Victoria Laurean, Said Malat Lyangana, Iman Paul, Faraji Yusuph, na Lin Zhang.
Wengine ni Sauli Epimark, Zacharia Mlacha, Eunice Ndirangu, Mtani Njegere, Zaituni Shillah, Dk Alice Simwinga na afisa wa kwanza wa ndege hiyo, Peter Odhiambo.
Hakuna miili mingine iliyopatikana. Taarifa za awali zilieleza kuwa ajali hiyo ilitokana na hali mbaya ya hewa. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesitisha shughuli zote za ndege katika uwanja wa ndege wa Bukoba kwa muda usiojulikana.
Shirika la ndege la AirTanzania, pia limesitisha safari zake Jumapili kuelekea Bukoba.
Timu ya wataalamu kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwa sasa ipo mjini Bukoba kuchunguza tukio hilo


