Wabunge wa Bunge la Afrika (PAP) wakiwa wamesimama kwa dakika moja kuwakumbuka Watanzania waliofariki dunia kwenye ajali ya ndege ya Kampuni ya Precision Air iliyotokea nchini Tanzania Jumapili Novemba 6,2022 katika Ziwa Victoria baada ya kushindwa kutua katika uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera. Picha na Kadama Malunde – Midrand Afrika Kusini
Rais wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament – PAP), Mhe. Chifu Fortune Charumbira akiongoza Mkutano wa Bunge la Afrika leo Jumatatu Novemba 7,2022
Rais wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament – PAP), Mhe. Chifu Fortune Charumbira (kushoto) akimpa pole Mbunge wa Bunge la Afrika kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anatropia Theonest kwa niaba ya Serikali ya Tanzania kufuatia ajali ya ndege ya Kampuni ya Precision Air iliyoua watu 19 baada ya kuanguka katika Ziwa Victoria Nchini Tanzania
Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wote wametuma salamu zao za faraja kwa familia za waathirika wa ajali hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Albert Chalamila ametaja marehemu kuwa ni pamoja na Neema Faraja, Hanifa Hamza, Aneth Kaaya, Victoria Laurean, Said Malat Lyangana, Iman Paul, Faraji Yusuph, na Lin Zhang.
Wengine ni Sauli Epimark, Zacharia Mlacha, Eunice Ndirangu, Mtani Njegere, Zaituni Shillah, Dk Alice Simwinga na afisa wa kwanza wa ndege hiyo, Peter Odhiambo.
Hakuna miili mingine iliyopatikana. Taarifa za awali zilieleza kuwa ajali hiyo ilitokana na hali mbaya ya hewa. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesitisha shughuli zote za ndege katika uwanja wa ndege wa Bukoba kwa muda usiojulikana.
Shirika la ndege la AirTanzania, pia limesitisha safari zake Jumapili kuelekea Bukoba.
Timu ya wataalamu kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwa sasa ipo mjini Bukoba kuchunguza tukio hilo

By Jamhuri