Na Heri Shaaban, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Isimail Ally Ussi, amesema Wilaya ya Ilala imeng’ara kwa mradi wa Nishati safi ya kupikia ya gesi katika soko la Kimataifa la Samaki Feri Wilaya ya Ilala .
Kiongozi wa mbio za Mwenge Isimail Ally Ussi, alisema hayo wilaya ya Ilala katika mradi wa nishati safi soko la Kimataifa Feri Dar es Salaam.

“Nawapongeza Madiwani, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo na Mkurugenzi wa jiji la Dar es Eriuma Mabelya kwa usimamizi wa mradi vizuri kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri Imail ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan “alisema Isimail .
Alisema soko la Samaki la Kimataifa Feri linatunza mazingira linaenda kuunga mkono juhudi za kampeni safi ya Rais Samia, katika masuala ya Nishati safi ya kupikia ambapo alisema awali nchi yetu ilikuwa mwenyeji wa mkutano wa masuala ya nishati.
Akizungumzia sekta ya afya mradi wa hospitali ya kisasa Mzinga alisema Rais Samia alitoa maelekezo mbali mbali kuwawezesha wananchi kiuchumi kujenga vituo vya afya ambapo alisema kituo cha afya Mzinga kinafana na hotel ya kimataifa ya nyota tano rais amefanya makubwa katika kituo cha Mzinga.

“Nampongeza Mkuu wa wilaya Edward Mpogolo, Meya wa jiji Omary Kumbilamoto,Madiwani na Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam nawaomba wananchi wakitunze na kukilinda”alisema Isimail.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo alisema kituo cha afya cha kisasa Mzinga kimejengwa kwa thamani ya shilingi bilioni 4 kitakuwa na wataalam bingwa .
Mpogolo akizungumzia ujenzi wa barabara ya Banana Kivule alisema hivi karibuni Serikali inatarajia kuanza rasmi ujenzi wa barabara hiyo mara baada mvua kumalizika yote hayo yanafanyika katika utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM.

Akizungumza mafanikio ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam alisema shilingi bilioni 18 zimeshushwa za mikopo kwa ajili ya vikundi vya wanawake vijana na watu wenye ulemavu kwa ajili ya kutoa mikopo.
Kwa upande mwingine alisema Jimbo jipya la kivule linatafuta mgombea ubunge ili aweze kucheza kalata zake aweze kwenda katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenda kuitetea Wilaya ya Ilala ikiwa na wabunge wanne.

