Na Tatu Saad,JamhuriMedia

Mshambuliaji kutoka DR Congo Jean Othos Baleke ameandaliwa Program maalum itakayomuongezea kasi ya kufunga mabao akiwa na Kikosi cha Simba SC, kinachojiandaa na mchezo wa Mzunguuko wasita wa Kundi C, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Programu hiyo maalum kwa Baleke ni katika kuhakikisha Mshambuliaji huyo anakuwa tishio katika Ligi ya Mabingwa Afrika, baada kuisaidia Simba SC kuchomoza na ushindi mkubwa wa 7-0 dhidi ya Horoya AC ya Guinea.

Kocha Mkuu wa Simba SC Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema anaamini ubora na kiwango cha Mshambuliaji huyo, lakini bado anahitaji vitu vichache vya kumuongezea, ili aendelee kuwa tishio katika Michuano ya kimataifa na Ligi Kuu Tanzania Bara.
Robertinho amesema tayari ameanza kumpa Program hizo Baleke tangu timu hiyo, ilipoingia kambini Ijumaa (Machi 24) huko Ndege Beach nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Licha ya Baleke kufunga mabao mawili katika mchezo uliopita dhidi ya Horoya AC, lakini anahitaji kutengenezwa zaidi ili kuhakikisha anazitumia nafasi nyingi ambazo anazozipata.”

Robertinho ameongeza SIMBA SC ipo katika mashindano makubwa hivyo lazima waweke sawa baadhi ya mambo ilinkuwa bora kila sehemu anamuongezea Baleke baadhi ya vitu ili aweze kufunga zaidi kwani ana kiwango bora sana.

“Ninataka kumuona Baleke akiendelea kufunga zaidi katika michezo ijayo, hilo linawezekana kwake kwani ana kiwango bora,” amesema Robertinho.

Baleke ni kati ya wachezaji waliosajiliwa Simba SC, wakati wa Dirisha Dogo msimu huu kwa ajili ya kuiongezea nguvu safu ya ya ushambuliaji ya klabu hiyo

By Jamhuri