Na Mwandishi Wetu,JmahuriMedia,Babati

Mmoja kati ya wagombea wa nafasi ya uwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Babati vijijini Ezekiel Dangalo ameamua kujitoa katika uchaguzi kwa madai ya kuwa na hofu ya kushindwa baada ya kushindwa katika uchaguzi wa awali.

“Nimeamua kujiondoa baada ya kuona vichwa ni vilevile vilivyonipiga vibaya kwenye uchaguzi wa awali hivyo nimeogopa” amesema mgombea huyo.

Hata hivyo kwa mujibu wa katiba ya chama cha mapinduzi, mgombea haruhusiwi kujiondoa siku ya uchaguzi, hivyo wajumbe wanaweza wakaamua kumchagua ama wasimchague.

Leo oktoba 2,2022 Chama cha Mapinduzi kinachoongozwa na Mwenyekiti wake wa taifa Samia Suluhu Hassan, kinafanya uchaguzi kuchagua viongozi katika ngazi za wilaya ambao wataongoza kwa kipindi cha miaka mitano.