Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), linaunga mkono maono na maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuvutia uwekezaji nchini kwa kuruhusu sekta binasfi ambayo ni injini ya kuleta na kujenga uchumi wa Taifa.

Katika utekelezaji huo NHC inatarajia kuzindua Sera ya Ubia iliyoboreshwa na kwamba maboresho hayo yamezingatia maslahi ya wabia, NHC na Taifa kwa ujumla.

Meneja Habari na Uhusiano wa NHC ,Muungano Saguya amesema kuwa uzinduzi huo unatarajia kufanyika kesho Novemba 16,2022 katika ukumbi nwa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi anatarajia kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Saguya amesema kuwa kutokana na taarifa hizo kumekuwa na muitiko mkubwa wa makampuni binafsi ya ndani na nje ya nchi kwa kutaka kushiriki uzinduzi huo ambapo washiriki 1,000 kutoka taasisi mbalimbali, bodi za kitaaluma, vyama, wawekezaji na Serikali wanatarajia kushiriki.

“Balozi zaidi ya 20, taasisi za kimataifa 10,Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, wenyeviti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), mawaziri, mhimili wa mahakama,tTaasisi za fedha na wawekezaji wa nje na ndani ya wamekubali kushiriki,” amesema.

Kutokana na utayari mkubwa wa makapuni na taasisi binafsi ndani na nje ya nchi kutaka kuwekeza katika ujenzi wa majengo makubwa kwenye viwanja vya NHC limeamua kuchambua na kuanisha maeneo yatakayokidhi shauku ya wawekezaji kwa kujenga nchi yetu.

“Hapo awali tulitenga maeneo 60 tu yenye viwanja/majengo yanayohitaji kuendelezwa. Kwa msukumo uliopo sasa tumeamua kuongeza maeneo zaidi ili yaendelezwe”

Vilevile katika uzinduzi huoa shirika limeandaa vitabu maalumu mahsusi kuelezea sera ya ubi ana maeneo ya uwekezaji ili kutoa taarifa zote muhimu kwa wawekezaji .

“ Tumejipanga vema siku hiyo ya uzinduzi ambapo kutakuwa na vyumba 12 Vilivyoandaliwa kupokea maoni ya wawekezaji na kuwapa maelezo watakaohitaji.”

Sera ya ubia ambayo tunawaalika Wawekezaji kushiriki ilianzishwa na Shirika tangu mwaka 1993 na kufanyiwa maboresho kadhaa kulingana na wakati husika.

Maboresho ya mwisho yalifanyika mwaka 2022 ili kuondoa changamoto zilizojitokeza hapo awali. Tangu kuanza kwa utaratibu huu, jumla ya miradi 111 ilitekelezwa ikiwa na thamani ya sh. Bilioni 300. Katika miradi hiyo, miradi 81 yenye thamani ya shilingi bilioni 240 imekamilika na kuanza kutumika na miradi 30 yenye thamani ya sh. Bilioni 60 inaendelea kukamilishwa

By Jamhuri