Rais Magufuli ametangaza msamaha kwa wafungwa 8,157 ikiwa ni kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kati yao, wafungwa 1,828 watatoka leo na 6,329 wamepunguziwa muda wa adhabu.
Miongoni mwa Wafungwa hao waliopata msaha wapo pia wafungwa 61 ambao walikuwa wamehukumiwa kunyongwa ambao wamekaa gerezani kwa zaidi ya miaka 40.
“Wafungwa walioko kwenye magereza hapa nchini ni wanaume 37,000 na wanawake 2000. Katika hili najua wanawake hawawezi kuomba usawa wa 50 kwa 50.” Magufuli alisema

1419 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!