Rais Mstaafu Karume awakumbusha wafanyabiashara kutoa risiti za kielektroniki

Na Rahma Khamis Maelezo Zanzibar

Rais Mstaafu wa Awamu ya Sita Dkt. Amani Abeid Karume amewataka wafanyabiashara kutoa risiti za kielektroniki na wanunuzi kudai risiti  li kwenda na mabadiliko ya teknolojia.

Dkt. Karume ametoa wito huo katika Uwanja wa Maisara wakati akifungua tamasha la tisa la biashara ikiwa ni shamra shamra za kuelekea kutimiza Miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema risiti ni kitu muhimu katika biashara kwani inasaidia kuhifadhi upotevu wa fedha pamoja kumrahisishia mfanyabiashara kuweka mahesabu ya bishara zake.

Aidha amefahamisha kuwa kuongezeka kwa matamasha kama hayo kunaimarisha fursa ya wafanya biashara jambo ambalo linaimarisha uchumi wa Zanzibar.

Rais Mstaafu wa Zanzibar awamu ya Sita DK,Amaan Abed Karume akitoa zawadi kwa Kampuni ya Azania Benk kwa Ushiriki wao na Mchango wa Mkubwa katika Ufunguzi wa Tamasha la Tisa la Biashara  linalofanyika katika Viwanja vya Naisara .Ikiwa shamra shamra za miaka  59 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Aidha Rais Mstaafu wa Awamu ya Sita amewaasa wafanyabiashara kuacha kufanya udanganyifu kwa kupunguza vipimo au kuzidisha kwa lengo la kujipatia kipato jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya  nchi na dini.

Hata hivyo ameishauri Wizara ya Biashara na Maendeleo ya viwanda kufanya tathmini ya matatizo yaliyojitokeza katika tamasha hilo ili kuyafanya matamsha mengine kuwa bora zaidi .

Naye Waziri wa Wizara hiyo Omar Said Shaaban amesema kuwa kufanyika kwa tamasha hilo ni moja ya utekelezaji wa Serikali katika kuhamasisha uchumi wa biashara ili kuwa na mvuto wa kukuza mazingira ya kibiashara.

Baadhi ya Wageni Waalikwa waliohudhuria katika Ufunguzi wa Tamasha la Tisa la Biashara  linalofanyika katika Viwanja vya Naisara .Ikiwa shamra shamra za miaka  59 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Aidha amefahamisha kuwa Serikali imeanzisha Tamashahilo kwa lengo la kuwafanya  biashara kuimarika zaidi kibiashara na kujiongezea kipato chao na taifa .

Ameeleza kuwa Serekali inaendelea kuhakikisha kuwa inakuza mazingira ya biashara kwa kutafuta eneo la kudumu Nyamanzi ili wafanya biashara waweze kuimarisha biashara zao zaidi.

Hata hivyo Waziri huyo amezishukuru taasisi za Serekali na wafadhili mbalimbali ambao wameshirikiana na kwa pamoja kwa kutoa michango yao kuhakikisha Tamasha hilo linafanyika.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ali Khamis amesema kuwa kufanyika kwa Tamasha la biashara ni kuwasaidia wafanyabaishara ili kubadilishana uzoefu wa kutengeneza bidhaa bora zaidi.

Aidha amefahamisha kuwa tamasha hilo limegharimu zaidi ya Shilingi milioni 277 ambazo zinatokana na michango ya wafadhili.

Rais Mstaafu wa Zanzibar awamu ya Sita DK, Amaan Abed Karume akisisitiza jambo wakati akitoa Hotuba ya Ufunguzi wa Tamasha la Tisa la Biashara  linalofanyika katika Viwanja vya Naisara .Ikiwa shamra shamra za miaka  59 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Katibu Mkuu huyo ameeleza kuwa tamasha hilo linapata hadhi kila mwaka kutokana na kukuwa kwake na kupata wageni kutoka maeneo mbali mbali .

Tamasha la biashara limewashkisha wafanya biashara mbalimbali wakiwemo kutoka  ndani na nje ya nchi ambapo kauli mbiu ya mwka huu USHIRIKISHWAJI WA JINSIA KWA MAENDELEO YA BIASHARA.

Rais Mstaafu wa Zanzibar awamu ya Sita  DK ,Amaan Abed Karume akitoa Hotuba katika hafla ya Ufunguzi wa Tamasha la Tisa la Biashara  linalofanyika katika Viwanja vya Naisara .Ikiwa shamra shamra za miaka  59 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais Mstaafu wa Zanzibar awamu ya Sita DK ,Amaan Abed Karume akikata Utepe kuashiria Ufunguzi wa Tamasha la Tisa la Biashara  linalofanyika katika Viwanja vya Naisara .Ikiwa shamra shamra za miaka  59 ya Mapinduzi ya Zanzibar.