Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo amemtembelea na kumjulia hali Mhe. Dkt. Salim Ahmed Salim nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam mara baada ya uzinduzi wa Tovuti ya Hifadhi ya Nyaraka za Kumbukumbu za Kidigitali za Kiongozi huyo kwenye hafla iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam tarehe 30 Septemba, 2023.

By Jamhuri