Watoto saba wamezaliwa katika mkesha wa Sikukuu ya Pasaka huku katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro.

Hayo yamebainishwa leo Jumapili April 9, 2023 na Kaimu Afisa Mahusiano wa hospitali hiyo, Scolastika Ndunga amesema kuwa watoto saba wamezaliwa katika mkesha wa Pasaka ambapo mmoja alifariki.

“Watoto saba wamezaliwa katika mkesha wa sikukuu ya Pasaka watoto wa kike watano na wa kiume wawili.

“Kina mama wawili wamejifungua watoto wao kwa njia ya upasuaji na watano njia ya kawaida”amesema.

By Jamhuri